Pages

Tuesday, March 18, 2014

Odama Jennifer Kyaka Kuwasaidia Wasanii Chipukizi.

Odama
Star mkubwa wa filamu nchini Odama Jennifer Kyaka amelijibu swali la shabiki wake Aman Wawi aliyeuliza ni vipi atasaidia wasanii wachanga ambao hawajui pakutokea. swali lilisema ,Vipi kuhusu kutusaidia watu kama sisi wenye vipaji asilia lakini bado hatujapata sapoti?


Odama amejibu "Soon tu nitakuwa na kundi la mazoezi ambalo litakuwa special kwa ajili ya kuwasaidia wasanii wachanga wanaohitaji msaada wangu maana ni ngumu sana kumsaidia mmoja mmoja tu anayepiga simu bila kumuona na kujua uwezo wake wa sanaa, kwahiyo kuanzisha sehemu ya mazoezi ndiyo itakuwa sehemu ya solution kwao"

Kwa upande mwingine Odama amesema kuwa filamu yake mpya kali inayoitwa JICHO LANGU itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu hivyo usikose nakala yako halisi ya filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya J-Film 4 Life inayomilikiwa na Odama

 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment