Pages

Wednesday, March 19, 2014

Wasanii Wakubwa Wanakwamisha Maendeleo Ya Kweli Katika Tasnia Ya Filamu Nchini: Liberty Msuya

Liberty
Liberty Msuya aliye muigizaji na producer wa filamu nchini Tanzania huku akiwa na makazi yake nchini Uingereza amefunguka mambo kadhaa kuhusiana na tasnia ya filamu wakati akichonga na Swahiliworldplanet. Star huyo wa filamu za Safari na Laura alifunguka wakati alipoulizwa mambo kuhusiana na usambazaji wa filamu nchini na kushawishi baadhi ya wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza katika sector ya filamu nchini. Liberty pia aliwatuhumu wasanii wakubwa nchini kuwa ndiyo wanakwamisha maendeleo ya kweli katika tasnia kutokana na kuingia mikataba uchwara na wasambazaji amabyo bado inaendelea kuwanyonya na kushindwa kuunganisha nguvu za pamoja na wasanii wenzao wengine ili kutetea maslahi yao.


Kuhusiana na kuwashawishi wawekezaji wa kusambaza filamu toka nje waje Tanzania Liberty alisema Bunge likikubali kuifanya sector ya filamu iwe rasmi ndiyo itakuwa na maana "labda mpaka bunge likubali ndio watu wanaweza kuja kuwekeza katika movies,.nahisi wasanii wakubwa ndio wanatuangusha nilitoa wazo la kuwa na chama cha ma-produser ambacho kipo ila hakina nguvu nikasema tukipe nguvu ili tuwe na wazo moja lengo moja na uamuzi wawote"

"Kama watengezaji movie watengenezaji movies tukisema hatuuzi master tunasema kwa wote kama tamko la watengenezaji movie bongo.then sokoni tushindane kwa kazi mzuri na sio walio na mikataka ndio wanaendelea na kuirudisha chini tasnia badala ya kuipeleka juu bongo movie, huwapromoti watu wao ambao wala sio wasanii wa kweli na kuacha wasanii wa kweli hilo ni latizo sugu"


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment