Pages

Saturday, March 15, 2014

Ukweli Kuhusu Amanda Poshy Kubakwa Huko Arusha Huu Hapa.

Amanda
Star wa filamu Swahiliwood Amanda Poshy ameanika ukweli juu ya skendo iliyoenea kama moto wa kifuu kuwa amebakwa jijini Arusha. Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Globalpublishers amanda aliitwa jijini Arusha na madogo flani waliodai ni wasanii chipukizi.

"Mwanzoni nasikia walihitilafiana kwenye malipo. Amanda alitaka Sh. milioni 2 lakini baadaye walikubaliana laki 8, Kweli Amanda alipofika Arusha alipokelewa vizuri na kupelekwa hotelini, Nasikia baadaye wale jamaa walimuibukia hotelini wakiwa watatu wakamtisha na kumbaka kisha wakaingia mitini. Kuna kipindi magazeti yaliandika anaumwa" kilidai chanzo hicho




Amanda ambaye anatamba na filamu mbalimbali sokoni alipotafutwa alisema "Huo ni uzushi uliotengenezwa na kijana aliyenipigia simu akaniomba nikacheze filamu yake lakini tulishindwa kuelewana, Walitaka nikacheze sehemu ya mhusika nkuu kwa laki 4 lakini niliwakatalia nikaawambia wafanye Sh. milioni 2"


"Walilalama sana wakidai ndiyo kwanza wanaanza hivyo wangeomba angalau nicheze vipande vichache. Tulivutana hadi nikafika Sh. laki 8 lakini walishindwa na kudai kuwa najiona niko juu hivyo nitaona, Hata kwenye ukurasa wangu wa Facebook, huyo jamaa amekuwa akinichafua. Ukweli ni kwamba sijawahi hata kuonana naye, (huku akimpigia simu mama na baba yake) mara yangu ya mwisho kwenda Arusha ilikuwa mwaka 2008. Kama hamuamini muulizeni mama na baba yangu. Sijawahi kubakwa katika maisha yangu"
Amanda
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment