Pages

Tuesday, March 4, 2014

Tanzania Inao Waigizaji Wengi Wazuri Kushinda Lupita Nyong'o Tatizo Ni Mfumo Mbovu.

Lupita Nyong'o
Pengine ninaweza kuwa blogger/media ya kwanza kutoka Tanzania kuweka habari kuhusu Lupita Nyong'o kupata nafasi ya kuigiza na wasanii wakubwa wa Hollywood katika filamu ya 12 Years a Slave mwanzoni kabisa mwa mwaka jana. Kipindi hicho dunia haikumjua Lupita ni nani ila watu wachache kutoka Afrika walikuwa wanamjua kupitia tamthilia ya MTV Shuga but hakupewa uzito na media akiwemo kwao Kenya ingawa bado wakenya walimtukuza kama star wao. Hata baada ya filamu yake kutoka bloggers na media nyingi za Tanzania hazikumuandika Lupita ila nilikuwa nikiweka updates zake mara kwa mara katika blog yangu hii kutokana na kumkubali tangu namuona mara ya kwanza hajawa maarufu.

Monalisa mmoja wa waigizaji wazuri nchini Tanzania
 Bloggers wengi na media nyingine za Tanzania zilianza kumuandika Lupita baada ya kuanza kupata tuzo mbalimbali kwenye film festivals na Award functions mbalimbali kupitia uhusika wake wa filamu ya 12 Years A Slave ambapo mwanzoni walimpuuza kumuandika au kumpa sapoti na watu kumjua zaidi ila media nyingi za nje hasa Hollywwod zilivyoanza kumuandika na wao wakaanza kumuandika na kumsifia huku wakimlinganisha na waigizaji wa Tanzania na kuwaponda waigizaji wa Tanzania ambapo hata hawawapi nafasi katika blogs au media zao kwa madai hawana viwango huku watu hao hao wakiwatukuza wanigeria ambapo kusema kweli filamu zao hazina tofauti na zetu za Tanzania tofauti ni lugha tu kwa asilimia kubwa.

Nimeanza kuandika kuhusu Lupita kuonyesha ni jinsi gani media za Tanzania hupuuza wasanii wa nyumbani na kutukuza pale media za nje zinapoanza kuwapa sifa kama ilivyokuwa kwa Lupita ambaye ni mkenya na jirani yetu sisi watanzania. Tangu Lupita ashinde tuzo kadhaa na baadaye tuzo ya Oscar(best supporting actress) baadhi ya bloggers, media nyingine na watu wa kawaida wamekuwa wakiwaona waigizaji wa Tanzania si kitu na kuwaponda sana. But bila kigugumizi nasema kuwa Tanzania tuna waigizaji wazuri sana kumshinda hata Lupita tatizo ni mfumo mzima wa tasnia yetu ambapo serikali inahusika sana kwa kupuuza na ndiyo hiyo hiyo pia leo inampongeza Lupita wakati haifanyi juhudi za dhati kuiinua tasnia ya filamu nchini. baadhi ya wasanii hawajitambui lakini wapo wasanii kibao wanajitambua nchini sema wanashindwa kupata support nje ya uwezo wao.

Lupita ana kipaji na elimu yake pia imemsaidia na ikumbukwe kuwa unapokwenda chuo cha sanaa hufundishwi kipaji bali kipaji unakuwa tayari unacho ila unaongezewa tu maarifa. Vile vile mpaka kufikia alipo sasa team nzima ya filamu ya 12 Years A slave imehusika sana kumfikisha alipo akiwemo mwandishi wa character yake na director aliyemuongoza vizuri yaani Steve McQueen. Lupita pia amejipatia umaarufu kupitia fashion kutokana na kuvaa vizuri kwenye matukio mbalimbali kiasi cha kuwavutia fashion critics wengi na media, hapa Tanzania bloggers wa fashions kumuandika muigizaji wa Tanzania ni kazi sana haileweki ni kwanini ila nina uhakika hawa wasanii wetu wanaopuuzwa sasa ikatokea bahati wakachomoka kama Lupita na kuandikwa na media za nje basi na media za Tanzania na bloggers nao wataanza kuwaandika usiku na mchana ! huu ni utumwa na kutothamini cha kwako.

Magazeti ya udaku nchini yameshupalia kuandika habari za wasanii wasio na vipaji ambao muda wote wako busy na vitendo vya kikahaba na kutengeneza skendo za uongo ili wajipatie umaarufu huku wakiacha kuwapa nafasi kabisa wale wasanii wenye vipaji vya kweli ambao ni rahisi kututangaza kimataifa kama Lupita wakipata nafasi. Ikumbukwe kuwa Lupita amepewa nafasi zaidi na media za marekani na nyinginezo kutokana na performance yake nzuri na sio skendo kama yalivyo magazeti ya burudani na udaku Tanzania, na kingine kilichomuongezea umaarufu ni media za fashion kumkubali anavyovaa.

 Tupende vya kwetu na kuwapa moyo na kutoa support kwa wasanii wetu  na sio kupongeza pale wageni wanapoanza kupongeza na sisi ndiyo tupongeze, tuthamini vipaji vya kweli vitakavyoipeleka tasnia yetu mbali na sio wauza sura. media zetu ziwe critical na wasanii wa kweli sio wababaishaji wasio na talent. Tunao waigizaji wazuri sana level za Lupita na hata kumpita wakipewa nafasi na kupata waongozaji wazuri wenye weledi kama alivyopata Lupita, Wasanii kama Monalisa, Lulu, Irene Paul, Gabo, Kemmy, Mariam Ismail, Jackson Kabirigi, Mohamed Musa na wengineo wanavyo vipaji na sifa nyingi tu za kuwika kimataifa, kinachotakiwa wajue kucheza na mabadiliko ya dunia ya sanaa ya filamu huku wakiweka mbele suala la elimu ambalo pia ni muhimu ingawa wapo waigizaji wakubwa kibao hata huko Hollywood hawana elimu ya chuo kikuu, ila kutambua lugha kadhaa hasa kiingereza ni muhimu kwa msanii kwa ajli ya mawasaliano na wasiojua kiswahili.

 Diamond Platinumz mwanzoni alipondwa sana na watanzania kuwa hana elimu na hatafika popote lakini ameamini kuwa anaweza na ndiyo maana licha ya kuishia kidato cha nne kielimu lakini kwasasa ndiye msanii wa Bongofleva wa Tanzania anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, management yake ipo makini na ina upeo mkubwa kitu ambacho kinatakiwa pia kwa wasanii wetu wa filamu.

Mwisho ikumbukwe kuwa 12 Years A Slave ni filamu ya Hollywood na sio ya Kenya hivyo kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima Lupita ang'are katika media za kimataifa nafasi ambayo hata Monalisa au msanii mwingine wa Tanzania akiipata leo ni rahisi kung'ara haraka kimataifa kama Lupita.

"ASIYEPENDA CHA KWAO NI MTUMWA"

                                                              Irene Paul
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

1 comment:

  1. Well said Amina ila penye ukweli ni lazima usemwe nahisi kwa upande mwingine elimu inasaidia katika tasnia ya filam pia nahisi filam nyingi Tanzania zina dhamira ambazo zinafanana ningeshauri tuwe wabunifu na kuandika vitu tofauti na mapenzi tujaribu kuchagua vitu vingine ambavyo vina mzunguka mtanzania pia naona movie nyingi hazijabeba uhalisia wa mtanzania mfano katika maisha ya mtanzania mtoto hawezi kukaa na kibukta au kimini mbele ya mzazi wake hasa wa kiume naona ni bora tuupende utamaduni wetu na kulenga soko la kimataifa pia watu wanaandika subtitles wawe wanaandika lugha ambayo.imekaa kitaaluma zaidi

    ReplyDelete