Meneja
wa Mradi wa Kusaka Vipaji Vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie
Talents) Bw Joshua Moshi akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wakutambulisha kampeni mpya ya kusaka Vipaji vya
uigizaji kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited mapema leo katika
Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino, Pembeni ni
Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Bw Evance Stephen
Meneja
Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (katikati)
akielezea jinsi ya Kampuni ya Proin Promotions itakapozunguka katika
Mikoa ya Tanzania Kwaajili ya Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania kwenye
Mkutano na waandishi wa Habari mapema leo katika Ofisi za Proin
Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino,, Shindano litaendeshwa na
Kampuni ya Proin Promotions Limited.
Meneja
Mradi wa Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents)
Bw Joshua Moshi (wa kwanza Kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Proin
Promotions Limited, Bw Evance Stephen wakisikiliza Maswali kutoka kwa
waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
leo katika Ofisi za Proin zilizopo Mtaa wa Ursino Mikocheni
Muigizaji
wa Filamu za Kitanzania Single Mtambalike almaarufu Rich Rich ambae pia
ni mmoja wa majaji katika Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lililopo chini ya Kampuni ya
Proin Promotions Limited akiongelea jinsi washindi watakavyopatikana
katika shindano hilo linalotarajia kuanza tarehe 1 Aprili 2014
Mwandishi
wa habari kutoka kituo cha Runinga Cha Channel Ten, Bw Fredy Mwanjala
akiuliza swali kwa Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents, Bw Joshua
Moshi (hayupo pichani) kuhusiana na Shindano la kusaka vipaji vya
uigizaji nchini
Meneja
Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (wa kwanza
kushoto) akionyesha stika za TRA ambazo zinaonyesha Uhalali wa filamu za
Proin Promotions lakini Pia Wateja watakaonunua Filamu kutoka Proin
Promotions wanatakiwa kutuma namba zilizopo kwenye stika hizo za TRA
kwaajili ya kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka Proin Promotions
kama Vile TV za Samsung na deki zake
Meneja
Masoko Wa Proin, Evance Stephen akionyesha Muhuri wa Moto uliopo kwenye
Kasha la Filamu kutoka Proin Promotions, Muhuri wa Moto, Kasha jembamba
na Stika za TRA ndio vitu vitatu vinavyooshesha Uhalali wa Filamu
kutoka Proin Promotions Limited
Wakijibu Maswali Kutoka Kwa Waandishi wa Habari
credit: Lukaza Blog
hawakusema hii kampeni itaanza lini?
ReplyDelete