Pages

Saturday, March 8, 2014

Je Unajua Kuwa Wastara Amezaa Na Mwanamuziki Solo Thang !

Wastara Juma ambaye ni star mkubwa wa filamu nchini anadaiwa kuzaa na mwanamuzki mkongwe wa Bongofleva nchini Solo Thang. Wastara ana watoto watatu na mmoja wao anadaiwa kuzaa na Solo Thang. Pia Wastara mwenyewe aliweka picha na maneno Instagram yanayodhihirisha hilo kuwa walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma wakati Solo akitamba katika Bongofleva kabla ya Wastara kuolewa na marehemu Sajuki baadaye.


Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema "Mtoto mmoja alizaa na Solo, wakati ule Solo akiwa anatamba na nyimbo zake kama Homa ya Dunia, Mambo ya Pwani na Mtazamo ambao alishirikiana na Afande Sele na Profesa Jay. Tena leo (juzi Jumatano) ameandika kwenye Instagram na ameweka na picha ya Solo"

Huko Instagrama Wastara aliandika " Baba wa baby wa miye, Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang, moyo wako haukupishana sana na wa Sajuki (Juma Kilowoko), Sijawahi kuyasema haya lakini utazipata salamu huko ulipo. Maisha yametutenganisha ila sijawahi kugombana na wewe wala familia yako. Nashukuru kwa upendo wenu juu yangu hasa mama yako. Nawapenda sana na hata mtoto wenu anawapenda. Dunia ni njia tu, hatujui nani atatangulia. Nakutakia mafanikio. Inshallah"

Waandishi wa GPL walipomsaka Wastara na kumuuliza kuhusu kuzaa na Solo Thang alijibu " Hivi kwa nini mnanifuatafuata sana jamani? Sasa umesema umeona Instagram, kwa hiyo nikusaidie nini?". Alipododoswa zaidi Wastara alijubu tena "Naomba mniache, nina mambo mengi yananisumbua kichwani mwangu. Kama wameona, acha waone(halafu akakata simu)"

                                                              Solo Thang

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment