1.WEMA SEPETU
Ni Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu nchini, Wema hakauki katika vyombo vya habari nchini kutokana na skendo za mara kwa mara au maisha yake binafsi na ya kimapenzi.
Power quotient: Filamu anayoigiza iwe mbaya au nzuri ni lazima iuze sokoni kutokana na kuwa na nyota ya kupendwa na watu wengi licha ya kuwa kipaji chake cha uigizaji kinatia shaka na wasiwasi.
2. LADY JAYDEE
Ni mtunzi wa nyimbo na mwanamuziki wa muda mrefu ambaye nyimbo zake nyingi zimekuwa hits, ana mashabiki wengi na nyimbo zake nyingi hata za zamani hazichuji.
Power quotient: Queen of Bongofleva, Wakati industry ya muziki wa Bongofleva ikionekana kushikiliwa zaidi na wanaume, Jaydee amedhihirisha kuwa kipaji anacho na ni jasiri kuliko mwanaume. Jaydee haogopi mtu yeyote yule anayemuwekea kauzibe mbele yake na kuzuia mafanikio yake. Mpaka sasa hana mpinzani wa kike katika muziki wa Bongofleva licha ya kuwa na zaidi ya miaka kumi kwenye game. She is the most successful "Anaconda" diva in the music industry.
3: FLAVIANA MATATA
Ni mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania akiwa na makazi yake nchini marekani, ameshatokea kwenye shows za designers wakubwa duniani na fashion weeks kubwa kama vile London na New York Fashion Weeks. Kupitia foundation yake ya Flaviana Matata anawasaidia wanafunzi mbalimbali wa msingi na secondary hasa wasichana mahitaji mbalimbali ya shule.
Power quotient: Role model wa wanamitindo wengi chipukizi nchini Tanzania na Africa kwa ujumla.
4. YVONNE CHERRYL "MONALISA"
Ni director, producer na muigizaji wa muda mrefu nchini Tanzania, tayari ameigiza filamu nyingi na anakubalika. Filamu yake ya Girlfriend ndiyo inadaiwa kuleta ushawishi na mapinduzi ya kutengeneza filamu za kibiashara nchini.
Power quotient: Endless Fame and talent, ni zaidi ya miaka 12 tangu Monalisa aanze kuigiza na kupata umaarufu na hawajawahi kuchuja tofauti na waigizaji wenzake wengi wa kike aliowika nao miaka hiyo ambao hawajulikani walipo huku wengine wakijikongoja kwenye tasnia. Monalisa pia anachukuliwa kama atress wa Tanzania mwenye sifa za kuwika kimataifa.
5.SALAMA JABIRI
Ni mtangazaji wa muda mrefu sasa alipijipatia umaarufu na na kipindi cha Planet Bongo na sasa Mkasi show vyote vikirushwa EATV.
Power quotient: Game changer...ingawa kwa sasa Salama hatangazi tena kipindi cha Planet Bongo lakini aliweza kuleta mapinduzi kwa wanamuziki wengi wa Bongofleva kufanya video nzuri kutokana na kuzikosoa video mbovumbovu bila kumuonea aibu mtu so wanamuziki wengi wakawa na hofu ya kufanya video zisizo na viwango kwa kuogopa kulipuliwa na salama. mpaka leo watu wanakumbuka mchango na nguvu ya bidada huyu.
6.RITA PAUSLEN(MADAM RITA)
Ni mwanzilishi wa shindando maarufu la kusaka vipaji nchini liitwalo Bongo Star Search aliyeibua vijana wengi kupitia shindano hilo.
Power quotient: Madam Rita ni kimbilio la vijana wengi wanaotaka kutoka kupitia muziki na kiuchumi lakini hawajui waanzie wapi so wanajitosa Bongo Star Search. Akiwa kama mwanamke ameweza kilisimamia shindano hilo na kusimama vizuri tangu lianzishwe mpaka leo licha ya washindi wengi kushindwa kufurukuta baada ya kushinda.
7.MARIA SARUNGI -TSEHAI
Ni mwandaaji wa mashindano ya Miss universe, Miss Eath Tanzania ambaye ameibua vipaji vingi vya urembo kupitia mashindano anayoandaa.
Power quotient: Ameweza kuondoa kasumba kuwa warembo wa Tanzania hawafurukuti katika mashindano ya kimataifa kutokana na warembo wengi wanaoshinda katika mashindano anayoyaandaa kufanya vizuri kimataifa kuliko mwandaaji mwingine yeyote wa mashindano ya urembo nchini. Mfano. mzuri ni Flaviana Matata, Miriam Odemba na Tetemaria Mallya ambao waliingia final za mashindano ya kimataifa na kushika nafasi za juu.
8.LEAH MWENDAMSEKE(LAMATA)
Lamata ni writer na director maarufu wa kike nchini akichuana kwa ukaribu na directors wa kiume maarufu nchini. Ni vigumu kwa wanawake wengi kukubali uwezo wa mwanamke mwenzao hasa katika field inayoshikiliwa zaidi na wanaume kama uongozaji wa filamu lakini waigizaji wengi wakubwa wa kike nchini wanawakimbia directors wa kiume na kutaka kufanya kazi na mwanamke mwenzao. Ameongoza filamu nyingi zilizochezwa na na Nisha, Odama, Jackline Wolper na wengineo.
Power quotient: Ndiye director mwanamke maarufu na mwenye mafanikio zaidi nchini kwani filamu nyingi anazoongoza zinafanya vizuri sokoni.
9. Millen Magese.
Ni mwanamitindo wa kimataifa toka Tanzania akifanya kazi zake nchini Marekani na S.Africa na ameshafanya shows nyingi na designers tofauti wakubwa na pia kutokea kwenye majarida mengi ya mitindo Millen anaaminika kama mmoja wa mastaa wa Tanzania wa kimataifa asiyependa kujikomba na kujipendekeza kwenye media ili aandikwe kwa mambo yasio na maana. Huisaidia sana jamii ya watu wasiojiweza na mara nyingi hufanya hivyo kimya kimya bila kutaka umaarufu kwenye media.
Power quotient: Inspiration ya models wengi chipukizi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wanaotaka kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa mitindo. Mmoja wa wanamitindo wa kwanza kabisa kuonyesha kuwa Tanzania inaweza kufanya modelling kimataifa na mpaka sasa bado anafanya vizuri.
10. ODAMA JENNIFER KYAKA
Odama ni actress maarufu wa kike nchini ambaye pia ni producer akiwa tayari amecheza na kuandaa filamu zaidi ya 14 na kufanya vizuri sokoni. Kampuni yake pia inakodisha vifaa vya kushutia filamu kwa waandaji wengine.
Power Quotient: Producer wa kwanza mwanamke mwenye mafanikio ambapo hata waigizaji wenzake wa kike wenye majina makubwa wanajifunza kwake na kumchukulia kama mfano wa kuigwa katika field ambayo bado inashikiliwa na wanaume.
11. JOKATE MWEGELO
Ni muigizaji wa filamu, mwanamitindo, mbunifu, mjasiriamali na mtangazaji, amejizolea sifa kama mmoja wa mastaa wanaojiheshimu nchini.
Power quotient: Mtangazaji wa Tanzania wa burudani wa kimataifa kupitia Channel O.
12. DJ FETTY
Mtangazaji wa kipindi cha XXL na Dj anayewakuna mashabiki wengi.
Power quotient: Dj mwanamke maarufu zaidi na anayekubalika kikazi.
13. ELIZABETH MICHAEL "LULU"
Lulu amekulia katika Tv na kujipatia umaarufu tangu akiwa bado mtoto mdogo kupitia Kaole. Ana uwezo mkubwa wa kuigiza na amejaaliwa mvuto pia, kama akipata mangement nzuri Lulu ni rahisi kuwika hata nje ya Afrika. Ameigiza filamu nyingi na ni mmoja wa waigizaji wa kike anayeuza sana na habari zake kufuatiliwa sana na mashabiki wa burudani nchini.
Power quotient: Lulu bado yupo juu kwenye filamu kila mtengeneza filamu anataka kufanya nae kazi hata baada ya kukumbwa na misukosuko ya kuhusishwa na mauaji ya Steven Kanumba bila kukusudia. Wengi walitarajia Lulu kuporomoka katika filamu baada ya kutoka segerea lakini alijipanga vziuri, kujipa moyo na kutokata tamaa baada ya misukosuko ya segerea. Licha ya kuwa na umri mdogo lakini amehimili mengi na kuwa juu that is what we call woman strength and power.
14. VANESSA MDEE
Mtangazaji na muimbaji wa muziki wa kizazi kipya.
Power quotient: Mtangazaji wa kwanza kutoka Tanzania kufanya kazi za kimataifa na MTV huku akiwahoji wanamuziki wakubwa wa Marekani kama vile Rick Rose, Kelly Rowland, Ludacris na wengieno.
15. JACKLINE WOLPER
Ni producer na muigizaji wa kike mrembo mwenye muonekano wa kistaa nchini, Wolper amecheza filamu nyingi sana na kujijengea jina kupitia uigizaji.
Power quotient: From Kanumba, Ray and JB kwasasa Wolper yupo juu sana na kuwa busiest actress na shooting, kila producer anataka kufanya nae kazi huku filamu zake zikifanya vizuri sokoni pia.
16. EVELYN RUGEMALIRA.
Ni fashion designer maarufu nchini ambaye alitwaa tuzo ya Swahili Fashion Week 2014 kama designer bora wa mwaka.
Power quotient: Designer wa Tanzania mwenye products zenye ubora wa kimataifa, kuanzia designs, materials mpaka finishing, products za Eve Collection ni za ubora wa hali ya juu kiasi cha celebrities wakubwa Tanzania kama vile Wema Sepetu na Madam Rita kuvaa nguo za Eve Collections katika red carpet za events mbalimbali. Hata wale fashionistaz wa Hollywood wakiona kazi za Eve Collection hawatasita kununua kwa ajili ya mitoko ya ukweli.
17. RIYAMA ALLY
Ni muigizaji wa muda mrefu sasa anayekubalika sana kwa wapenzi wa filamu za Tanzania.
Power quotient: Kipaji chake ndiyo imekuwa silaha kubwa ya watengeza filamu wengi kutaka kufanya nae kazi kutokana na kukubalika kwa mashabiki wengi. Baadhi ya waigizaji wa kike hupewa nafasi za kuigiza kutokana na muonekano wao wa kisista duu bila kujali kama wana vipaji au lah lakini kwa Riyama kipaji alichojaaliwa ndiyo silaha yake ya kutamba kwenye filamu.
18. SALMA JABU NISHA
Ni muigizaji wa filamu ambaye hana muda mrefu katika tasni ya filamu nchi lakini amekubalika haraka na kujizolea mashabiki wengi. Nisha anamiliki kampuni yake ya filamu pia.
Power quotient: Serious-comedy queen , tofauti na waigizaji wengi wa kike ambao hutamba aidha kwenye vichekesho au uigizaji serious pekee Nisha yeye ameweza kutamba kotekote kwenye filamu serious na za comedy na kufika kileleni wanapopataka wengi. Tikisa na Gumzo zimepokelewa vizuri sana sokoni na kumuongezea mashabiki wengi Nisha.
19.LUCY KOMBA
Ni mwandishi, producer, director na muigizaji wa muda mrefu aliyejipatia umaarufu kutokana na kipaji chake cha filamu tangu akiwa Kaole Sanaa Group na baadaye kwenye filamu. Lucy pia anamiliki kampuni yake ya filamu.
Power quotient: Lucy Komba anaaminika kuwa producer wa kwanza wa kike nchini kabla ya kuja producers wengine wa kike. Pia anasemekana kuwa actress wa kwanza Tanzania kutafuta channels za kimataifa na waigizaji wenzake wa mataifa mengine kama Ghana, Nigeria, Denmark etc. Amewatoa mastaa wenzake kibao wanaotamba sasa wakiwemo wanawake wenzake kama vile Jackline Wolper na Irene Uwoya. Hii ina maana kuwa kama Lucy Komba asingekuwepo katika filamu leo hii usingewajua pia Wolper na Uwoya. Lucy Komba ni kimbilio la underground wengi kutokana na kutokuwa na tamaa ya kutaka yeye pekee atambe katika filamu.
20. ASIA IDOROUS KHAMSIN
Ni designer wa muda mrefu sana ambaye ameshafanya fashion shows nyingi ndani na nje ya Tanzania kama vile Lady In Red na Usiku wa Khanga Za Kale.
Power quotient: Ingawa kuna fashion shows nyingi nchini lakini upcoming fashion designers wengi hutaka kuanza kuonyesha vipaji vyao zaidi kupitia shows za Asia Idorous ambaye huwachukulia kama watoto wake ndiyo maana hujulikana pia kama "Mama wa mitindo Tanzania"
21. WASTARA JUMA
Ni muigizaji wa muda mrefu anayekubalika kwa mashabiki wengi wa filamu nchini, tayari ameshacheza filamu nyingi sana, pia ni producer.
Power quotient: Kipaji chake ndiyo kimemfanya bado azidi kuwa juu licha ya kukumbwa na misukosuko kibao ikiwemo kukatwa mguu wake ambapo wengi walidhani ingekuwa mwisho wake wa kutamba katika tasnia ya filamu nchini lakini bado producers wengi wanataka kufanya nae kazi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuigiza.
22. SHAMIM MWASHA.
Ni blogger maarufu wa fashion akimiliki blog ya 8020fashions ambayo ina watembeleaji wengi wanaongalia mitindo mingi ya mastaa wa ndani na nje ya Tanzania anayoweka. Pia ndiye mwandaaji wa Women Celebration event nchini Tanzania ambayo inawakusanya wanawake wenzake pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na kujadili mikakati ya kimaendeleo.
Power quotient: Blogger wa kwanza wa fashion Tanzania kutoa inspirations kwa blogger wengine wa fashions nchini.
23: MANGE KIMAMBI
Pengine Mange Kimambi ndiye blogger wa Tanzania mwenye ushawishi mkubwa zaidi kwa kuvuta comments nyingi za wasomaji kwenye blog yake ya U-turn, blog yake inawatembeleaji wengi sana ambapo wengi huenda kupiga gossips na kufanya sehemu ya kutolea uchovu wanapokuwa wamechoka. Mange anaweka contents mbalimbali zikiwemo za mastaa wa burudani na fashions nchini. Mange kama ange-set vizuri programs za matangazo ya google na affiliates nyingine basi angejiingizia pesa nyingi kupitia blog yake kama ilivyo kwa Linda Ikeji an Bella Naija wa Nigeria.
Power quotient: blogger wa burudani wa kike Tanzania mwenye ushawishi mkubwa kwa wasomaji kiasi cha celebrities wengi nchini kupatwa na kiwewe cha comments za kuwachamba habari zao zinapowekwa katika blog hiyo.
24 CHRISTINE MANONGI "SINTAH"
Huyu ni muigizaji na blogger maarufu sana pia wa celebrities gossips na mwenye ushawishi mkubwa pia kwa wasomaji wengi. Blog yake ya Sintah inavuta wasomaji wengi kama ilivyo kwa Mange Kimambi. Sintah habanii comments za wasomaji wake kiasi cha kuzidi kuwavuta wengi kila siku ambapo huvutiwa na habari za gossips anazoweka na wao kuchangia na kujiona kama kijiji kimoja ndani ya blog hiyo, blog hiyo hutumiwa kama sehemu ya kundoa uchovu na stress za wasomaji wengi kutokana na comments zenye maneno ya kila aina ya kuwachamba mastaa wanaoenda ndivyo sivyo au kuwapongeza wanaofanya mambo mazuri. Sinta aki-set vizuri matangazo ya google na affiliates atajiingizia pesa nyingi kupitia blog yake tofauti na sasa, pia akiongeza habari zake kuwa nyingi kwa siku ni rahisi kuwa blogger anayesomwa zaidi Tanzania na pengine hata Afrika mashariki.
Power quotient: Celebrities wengi wa Tanzania huwa tumbo joto habari zao zinapowekwa katika blog ya sintah kwa kuogopa kuumbuliwa na kuchambwa hasa kwa wale wanaopenda ku-fake maisha na kufanya mambo yasio na maana wakiwa kama vioo vya jamii.
25.MISSIE POPULAR
Mariam Marion Ndaba ni blogger maarufu wa fashions nchini akimiliki blog ya Missiepopular. Pengine ndiye blogger mwenye uwezo na upeo mkubwa wa kuchambua habari za fashions za mastaa na watu katika events mbalimbali nchini. Blog yake huwa inatoa somo kabisa kwa wale wasiojua fashions ni nini na wapi nguo au fashion husika inaweza kuvaliwa na kwa wakati gani. Hata hivyo Missiepopular haandiki sana habari za mastaa na wanamuziki wa Tanzania ila kama angeziandika na kuwafuatilia sana katika kile wanachovaa na hata habari zao za kazi zao basi angejiongezea wasomaji wengi zaidi kutokana na blogs zinazotumia lugha ya kiingereza nchini kuwa chache huku yeye akiwa na uwezo mkubwa wa kuandika kupitia lugha hiyo.
Power quotient: blogger wa Tanzania mwenye uwezo mkubwa zaidi kuhusu fashions za celebrities, kupitia uwezo wake wa kukosoa na kueleza nini kifanyike Missiepopular ameweza kupunguza uvaaji mbovu kwa celebrities wengi na watu wa kawaida katika events kubwa kama vile Miss Tanzania.
good list
ReplyDelete