Sunday, March 2, 2014

Filamu Ya "Gumzo" Toka Kwa Nisha Yafanya Vizuri Sokoni, Yagombaniwa Kama Njugu.

Nisha
Habari ni kuwa star wa filamu nchini anayefanya vizuri kunako game la filamu Salma Jabu Nisha ameirudisha heshima ya filamu Tanzania baada ya kudaiwa kudorora hapo kati kwa mujibu wa wauzaji wadogowadogo. Machinga wa filamu za kibongo wanasema tangu "Gumzo" iingie sokoni imekuwa gumzo kweli na kuwa biashara nzuri kwao. Wauzaji hao wanadai Nisha anawafanya wauze biashara sana kuliko waigizaji wanaotoka magazetini kila siku huku sokoni filamu zao kudaiwa kutofanya vizuri.


Ukiachilia mbali Nisha filamu ya Gumzo imechezwa na mastaa wengine kama vile King Majuto, Hemedy, Wastara Juma, Tausi na wasanii wengine wenye vipaji. Hakikisha unapata nakala yako halisi.


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment