|
Sabby Angel |
Salma Tamim(Sabby Angel) ambaye ni muigizaji wa filamu Swahiliwood amekwaa skendo mpya ya kudaiwa kutembea na mume wa mtu huko Kenya na ndoa ya mwanaume huyo kuwa hatarini kusambaratika. Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka Mombasa, Kenya kikizungumza na
Swahiliworldplanet kilisema kuwa mwanaume huyo ni Hassan Faisal producer maarufu wa filamu nchini humo na mmiliki wa kampuni ya Coastal Films. Chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema kuwa mke wa jamaa huyo kwasasa anadai talaka yake mahakamani huku Hassan ambaye kiumri ni mkubwa sana kwa Sabby akidaiwa kuwa na ndoto za kuoa muigizaji wa filamu.
Wawili hao inadaiwa siku hizi kila Sabby akienda Kenya wanakuwa pamoja kama Kumbikumbi na kwenda pamoja kwenye viwanja mbalimbali vya burudani. "Sabby and Hassan Faisal are dating, me nawaona sana pamoja waki-party different places, mkewe Hassan anataka talaka yake, unajua yule Faisal ni filmmaker huku Kenya so he wants to marry an actress"
Baada ya kuzipata habari hizo wiki iliyopita
Swahiliworldplanet ilijaribu kumtafuta Hassan ili atolee ufafanuzi madai hayo na kutoka na Sabby lakini juhudi hazikuzaa matunda. Nae Sabby Angel alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo alijibu kwa ufupi kwa kusema " not true".
Hassan aliyevaa miwani akiwa na Sabby Angel na jamaa mwingine
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment