Akizungumza na Globalpublishers mama Wema alisema:
“Najua kwa sasa sina tena mamlaka ya kuingilia mapenzi ya binti yangu kwani mambo hayo yamenichosha, yananiumiza na kichwa.
“Lakini naomba sana kwa Mungu itokee siku moja Wema amfumanie Diamond akiwa na mwanamke mwingine labda ndiyo itakuwa kikomo chao cha kuwa wapenzi kwani ndiyo ndoto ninayoiota kila siku.”
KWA NINI ANAOMBA DUA BAYA?
Mama Wema alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba, amegundua binti yake huyo hana ubavu wa kuachana na Diamond hata kama atasikia ana mwanamke mwingine.
Mwanamke huyo anayemwogopa Mungu tu, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba, kuna wakati baadhi ya magazeti pendwa nchini yaliandika Diamond kuwa na demu mwingine lakini Wema hakukasirika wala kuachana na staa huyo wa muziki wa kizazi kipya.
“Kwa hiyo mchezo mzuri ni yeye (Wema) kumfumania huyo Diamond wake, maana magazeti tu kuandika kwamba ana uhusiano na mwanamke mwingine mwanangu alivyofanywa mjinga wa kutupwa, hatamwacha.
“Mimi najua Wema anashindwa kukaa chonjo kwa sababu ndumba zimemtawala, amefunikwa labda baadaye atafunguka,” alisema mama Wema.
AIGUSA SAFARI YA DIAMOND NCHINI NIGERIA
Mama Wema akaanika jambo ambalo halijawahi kujulikana kabla.
Alisema: “Huyo Diamond ndo maana alikwenda Nigeria akashindwa kupiga muziki kwa sababu hakwenda na Wema, sasa ameona ampumbaze ili aweze kwenda naye nchi za nje kwa masilahi yake binafsi, ataishia kumuahidi tu hana uwezo wa kumnunulia Wema kitu chochote chenye thamani kubwa, ni mpenda misifa tu.
“Si mnamjua huyo ni mtoto wa Tandale? Anajiita yeye m...(alitaja jina la kinyesi) na kweli yuko hivyo.
NDUGU WA DIAMOND WAMEJAZANA KWA WEMA
“Ndugu zake walivyo washamba wamejazana hovyo pale kwa Wema. Wajinga mno, maana mshamba siku zote ni mshamba,” alisema mama huyo.
HATAKI KUSIKIA WEMA ANA MIMBA YA DIAMOND
Katika hali iliyoonesha kwamba kweli hampendi Diamond, Bi. Mariam alisema hataki kusikia binti ana ujauzito wa msanii huyo.
Alisema: “Mbegu (uzao) gani atakayoileta kwangu, huyo mjukuu si atakuwa balaa, siwezi kuharibiwa wajukuu. Mtoto asiyeeleweka siwezi kumshika.”
ACHIMBA MKWARA
“Halafu nataka kuwaambia enyi watu wa magazeti, haya mambo ya kumwongelea huyo domo acheni mara moja, dunia itamnyoosha,” alisema.
AJIRUDI KWA MWANAYE
Mama Wema alisema hawezi kumlaumu sana binti yake kwa vile akili si yake, yeye (Wema) ni mwanake na atabaki kuwa mwanamke, ila siku zote lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.
DIAMOND SASA
Diamond alipotafutwa na GPL kwa njia ya simu na kumjulisha kuhusu ndoto za mama mkwe wake huyo aliishia kucheka.
“Teh! Teh! Teh! Thubutu.”
No comments:
Post a Comment