Thursday, January 9, 2014

WEUPE WA WEMA SEPETU WATOWEKA, NGOZI YAKE YA ASILI YAMRUDIA.

Star wa filamu Swahiliwood na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Wema Sepetu ameanza kurudia weusi wake wa zamani na ule weupe wa kichina(mkorogo) umeanza kutoweka kwa kasi kitu ambacho kinadaiwa kumridhisha Wema mwenyewe alieyejutia kujichubua baada ya madawa hayo kumdhuru na kwenda nchini China kufanyiwa marekebisho ya ngozi yake ili iwe kama zamani. Muigizaji mmoja aliye karibu na Wema kwa sharti la kutotajwa jina ameuambia mtandao huu kuwa Weupe wa Wema umepotea kwa kasi baada ya kupigwa marufuku asitumie tena mkorogo na daktari aliyemtibu China kwani mkorogo huzeesha mapema na kuondoa vitamini mwilini. Hata watu wa karibu na Wema wakiwemo ndugu zake wanadaiwa kufurahia muonekano mpya wa Wema ambao alikuwa nao zamani.

"Weupe wa Wema umetoweka ghafla na ule urembo wake wa asili wakati anashinda Miss Tanzania unarudi, sasa hivi Wema amekuwa mweusi baada ya kuacha mkorogo, ndugu na jamaa zake wa karibu pia wanampongeza akiwemo mpenzi wake Diamond, unajua hata baadhi ya mastaa wenzake walikuwa wakimcheka Wema na kumuita michirizi baada ya kuharibiwa na mkorogo, ila sasa Wema anaanza kupata furaha ya urembo wake na kujutia uamuzi wa kujikoboa" alisema star huyo huku akionyesha picha mpya ya Wema (hiyo hapo chini) akiwa na mdogo wake Diamond aitwaye Rommy Jones.

                                                 Wema Sepetu na Rommy Jones


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment