Tuesday, January 7, 2014

NIMEGUNDUA NIMEMKOSEA MUNGU KWA KUTUMIA MKOROGO: MAINDA

Mainda ambaye ni star wa filamu Swahiliwood amesema anaamini kwa dalili alizoanza kuziona, mwaka huu utakuwa ni wa faraja kwake. Akizungumza na Globalpublishers juu ya dira ya mwaka 2014, Mainda alisema mwaka jana aliamua kuokoka baada ya kubaini kuna mambo anamkosea Mungu na imani yake ni kwamba Mungu atamsamehe na kumfungulia milango ya neema.

"Nimegundua wapi nilikosea na kwa kuwa nimeamua kumuabudu Mungu kikamilifu, naamini kila kitu kitakuwa sawa. Nimeingia kwenye wokovu nikiwa kama mtoto mchanga, naendelea kukomaa.
Yapo ambayo nilikosea kama vile kutumia mkorogo lakini mwaka mpya na mambo mapya,” alisema Mainda.

                                                                     Mainda

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment