Thursday, December 5, 2013

YALIYOAJIRI KUTOKA AFROWOOD FILM FESTIVAL 2013 NCHINI DENMARK.

Afrowood Film Festival kwa mara ya kwanza ilifanyika katika ukumbi wa Culture Centre, Copenhagen,  nchini Denmark wikiend iliyopita na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa filamu. Na filamu za kiswahili ziliwakilishwa na wasanii kutoka VAD Production, Twaleb Entertainment. Wageni waalikwa kama vile Tanya Kersey kutoka Hollywood, Yvonne Hans(Uk/Nigeria), Obi Ikenna(Uk, Nigeria, Marie K. Gomez na wengineo walikuwepo na kufurahia kuziona filamu za kiswahili na za lugha nyingine . Wadau hao walibadilishana uzoefu na kujifunza zaidi kuhusu filamu.

Hata hivyo habari za uhakika ambazo SWP zimepenyezewa na chanzo makini ni kuwa licha ya waandaaji kufanikiwa katika mipango yote ya tamasha hilo la filamu lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini humo lakini watu wa kawaida hawakujitokeza ukumbini t na hata baadhi ya wasanii waliotarajiwa kuwepo kama vile Genevieve Nnnaji na Ramsey Nouh kutoka Nigeria hawakuwepo wakati ilitangazwa hivyo. Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikuwa ukumbini hapo ni kuwa sababu hiyo inaweza kuwa ni kwa waandaji kushindwa kufanya publicity ya kutosha licha ya mengine yote kwenda sawa, sababu nyingine inatajwa kuwa pengine kulikuwa na events nyingine kubwa hivyo matukio kuingiliana.

 "Waandaaji walikuwa na kila kitu kilichotakiwa kuwa nacho ili kwenda sambamba na hali halisi ya uandaaji wa Festival kubwa kama hii...lakini kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vilisababisha iishie kati na isimalizike kama ilivyopangwa.....ingawa wasanii wakubwa na maarufu  baadhi yao walifika na tuliwapokea kwa furaha kubwa sana..Lakini ukumbini kulikosa watu..nadhani kujitangaza kuliwaangusha au tarehe za matukio ziliingiliana sana na watu kutohudhuria kama walivyopanga.....lakini kikubwa zaidi kwa mtazamo wangu ni kwamba wasanii kama Genevieve Nnnaji na Ramsey Nouh walikuwa kwenye orodha ya kuwa hapa lakini hawakufika ....nahisi habari hizi ziliposambaa kwa haraka sana na kuwafanya washabiki wasije kama walivyotegemea...huu ni mtazamo wangu..lakini anyway tulifurahi na kuwa pamoja na wageni muhimu na tulialikwa pia Hotelini walipofikia na Wote kulifurahi sana na kupita kiasi" kilisema chanzo hicho kikichonga na Swahiliworldplanet 

Maoni ya SWP: Hii ni hali ya kawaida kwa event yoyote ile kwani hata wasanii wakubwa wa Marekani hukumbana na hali kama hii wakati mwingine kutokana na sababu mbalimbali hivyo ilikuwa hali ya kawaida kwa waandaji wa Afrowood na tunafikiri watajisahihisha makosa waliyofanya mwakani. Na pia kwa kuwa Tamasha(Festival) lina sura ya filamu kutoka nchi  zote za kiafrika yaani Afrowood(African films) basi itakuwa muhimu miaka inayokuja waandaji wajitahidi kualika wasanii, producers, directors, na wadau wengine kutoka nchi mbalimbali za kiafrika ili Tamasha liwe na nguvu zaidi isiwe kwa baadhi ya nchi chache tu au mbili tatu kwani tamasha litakosa uhai na kupuuzwa na wadau muhimu.

Tukiachana na hayo angalia baadhi ya picha za matukio ya Afrowood..............






Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment