Pages

Tuesday, December 10, 2013

RAY ANANIFANYIA FITINA KWASABABU ALINITONGOZA NIKAMKATAA: NORA

Nora
Muigizaji wa filamu Swahiliwood na aliyewahi kufanya vizuri kupitia kundi la Kaole Sanaa Group, Nuru Nassoro(Nora) amedai kuwa amekuwa akifanyiwa fitina na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi(Ray) kwa kuwa aliwahi kumtaka kimapenzi akamkataa.
 
Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm na kudai kuwa Ray amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya makampuni ambayo anapeleka kazi zake.
 
“Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi nimeshawahi kusikia wanasema, wakaniahidi sana mpaka nikawakubalia walichokuwa wanataka wao. Lakini yeye (Ray) alitanguliza movies zake, akasema ana movie zake sijui kitu gani..” amelalamika Nora.
 
  “Alishawahi..kitu ambacho kwangu kimeshawahi, sasa mimi sijui yeye ni alivyo au kwangu..ila mimi alinibania kwa sababu nilikuwa simtaki, akaniharibia kwa Mtitu. Kanumba kipindi kile alikuwa anamsikiliza sana Ray, akamwambia asifanye kazi na mimi. Hata Kanumba alikuwa ameelewana na mimi Ray akamwambia ‘achana naye’.” Nora ameiambia Filamonata.
 
Amedai kuwa wanaume wengi katika tasnia ya filamu wanamekuwa wanawanyanyasa wanawake kwa kuwata kimapenzi, na kwamba inakuwa ni mambo ya ndani ambayo sio rahisi kufahamika.
 
“Ikitokea hivyo inakuwa ni mambo ya ndani sana kiasi kwamba hata mwenzako anakwambia kwamba utaona kama utaendelea kuwa flani.” Nora amefunguka.
 
Nora amedai kuwa ana kazi nyingi lakini ameshindwa kuziingiza sokoni kwa sababu ya kubaniwa.
 
Hata hivyo Nora amesema ameshasamehe na anaendelea na kazi zake.
Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.

                                                                         Ray
,
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment