Thursday, December 26, 2013

MKOROGO WAMTIA ADABU WEMA SEPETU, NILIDHANI KUWA STAR LAZIMA UWE MWEUPE.

Wema Sepetu
Mwishoni mwa mwezi November mwaka huu SWP iliandika habari ya Wema Sepetu kujuta kutumia mkorogo na kuitamani ngozi yake ya awali baada ya kujeruhiwa na madawa hayo na kwenda China kufanyiwa marekebisho ya ngozi yake. Habari hiyo ilikuwa exclusive hapa SWP baada ya kutonywa na mtu wa karibu na Wema na kama hukuisoma habari hiyo isome HAPA.

Hata hivyo Wema Sepetu ameamua kufunguka mwenyewe live kuwa anajuta kutumia mkorogo licha ya meneja wake Martin Kadinda miezi kadhaa nyuma kukaririwa na gazeti moja akikanusha kuwa Wema hatumii mkorogo kabisa bali ni mabadiliko ya hali ya hewa tu ndiyo yamemfanya kuwa mweupe kupitiliza. Isome habari hiyo hapo chini kutoka Globalpublishers

MISS Tanzania 2006 aliye pia staa wa filamu nchini, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa, mkorogo umemtia adabu na anajuta kuutumia  mwilini mwake.
Akizungumza juzi na paparazi wetu ofisini kwake jijini Dar, Wema alisema  kuwa baada ya kwenda kliniki nchini China na kupata matatibu ya ngozi yake ambayo sasa imerudi kama mwanzo amejifunza kitu.

NI KITU GANI HICHO?
Wema alisema amejifunza kuwa, binadamu anatakiwa kuishi alivyoumbwa na Mungu, mambo ya rangi ya mwili hayana nafasi katika uwezo wa binadamu.

ALIAMINI USTAA NI LAZIMA UWE MWEUPE PEE!
Wema akatoa mpya zaidi aliposema kuwa, uamuzi wake wa kutumia mkorogo ili awe mweupe kama mzungu (yeye ni mweupe) ulitokana na kuamini kwamba, weupe na ustaa ni mambo yanayokwenda pamoja, kumbe sivyo.
“Niliamini weupe sana na ustaa ni Kulwa na Doto, lakini sivyo. Ngozi yangu ya awali ni nzuri, imerudi kama ilivyokuwa, namshukuru sana Mungu,” alisema Wema.

AWAONYA MASTAA WENZAKE
Akiendelea kuzungumza na paparazi, Wema alitoa ujumbe kwa mastaa wenzake wanaotumia mkorogo kuwa, hakuna faida yoyote, kwa sababu mkorogo unaondoa vitamini yote mwilini.
“Daktari kule China aliniambia kuwa licha ya kupoteza vitamini nyingi mwilini, pia mkorogo unakufanya mtu uzeeke kabla ya  wakati. Mimi nawaomba kabisa mastaa wenzangu wajiepushe na hii kitu inaitwa mkorogo,” alisema Wema.

ALICHOJIFUNZA KUHUSU KUJIKOBOA
Kujikoboa ni kuwa mweupe sana, lakini Wema anasema alichojifunza kuhusu hali hiyo ni kwamba, ni rahisi sana kuiondoa ngozi ya awali kwa mkorogo lakini inapofika ngozi ya awali inatakiwa kurudi inagharimu sana.
“Ukitaka kuona maajabu sasa, ngozi yako mwenyewe kuibadilisha si kazi na wala si gharama lakini ukitaka irudi kama mwanzo ni lazima ugharimike sana, mimi sitaki tena jamani,” alisema Wema.

 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment