Saturday, December 21, 2013

DIANA KIMARO AJUTA KUJITANGAZA NI BIKIRA, WANAUME WAMSAKA USIKU NA MCHANA.

Takribani miezi kadhaa iliyopita star wa filamu Swahiliwood Diana Kimaro alikaririwa akisema kuwa yeye ni bikira na hajawahi kuduu na mwanaume yeyote kwani yupo busy na shule. Diana aliyasema hayo katika kuweka wazi kuwa baadhi ya watu walikuwa wanamuona ni mcharuko kweli kutokana na baadhi ya filamu alizoigiza kama mcharuko na kucheza vizuri hivyo wengine kudhani ni kweli. Hata hivyo habari mpya kutoka chanzo kimoja ambacho kipo karibu na Diana zinasema kuwa Diana anajuta kusema kuwa ni bikira bado kwani baada ya habari zile kutoka na kuenea mitandaoni wanaume wamekuwa wakimsumbua sana kuliko hata mwanzoni ili kuonja penzi lake kwa mara ya kwanza.

" Diana anajutia uamuzi wake wa kujitangaza ni bikira, wanaume ndiyo wamezidi kumsumbua kuliko mwanzo tangu habari zile zienee kuwa bado ni bikira yaani anasakwa usiku na mchana, wanaume  ni watu wa ajabu sana na siwajua bado anasoma" Chanzo hicho kiliiambia Swahiliworldplanet

Mtoa habari hizo alipoulizwa tena kuwa anafikiri ni kweli Diana ni bikira?, kwanza aliangua kicheko cha haja na kujibu " sina jibu kamili yeye ndiyo anajua ukweli"

Hata hivyo Diana amabye ni star wa filamu za Family Disaster, After Death na Foolish Age alipotafutwa jana  ili kuelezewa kuhusu issue hiyo hakuweza kupatikana.

                                                                            Diana Kimaro

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment