Sunday, July 21, 2013

SHILOLE AAPA KUMFUNZA ADABU SINTAH BAADA YA KUMPONDA NA KUMDHIHAKI KUWA HAWEZI KUFANYA KAZI NA JENIFER LOPEZ.

Shilole

Shilole ambaye ni actress na pia mwanamuziki amemjibu Sintah na kuapa kumpa kipigo cha mbwa mwizi baada ya Sintah ambaye pia ni muigizaji wa filamu na pia mtangazaji wa Tv kumponda Shilole kuwa ni ndoto kwa Shilole kuimba pamoja na Jenifer Lopez(J.Lo) wa Marekani kama Shilole anavyodai kuwa muda si mrefu atafanya kazi na Lopez baada ya meneja wake kuvutiwa na kazi za Shilole aliyekuwa Marekani hivi karibuni na kumpelekea J.Lo kuziona. Akiongea na mtandao wa filamucentral kwa hasira Shilole alisema "Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi"

Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake, sehemu ya maneno yanayomkera Shilole ni haya
“Shilole bwana hii week katujia na kali kuliko eti ameongea na Benny Medina (Jlo’s Manager) ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua lakini swali ni?? wataimbaje?? yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado sijaujua ni chakacha ama nini sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa music, hili linauwezekano??,”
“ Chakacha na RnB?? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa sasa Shilole?? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi ktk reality,”

 Ameshangaa Baadhi ya watanzania kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia muziki wa Marekani wakati wenyewe hawana muda na muziki wa hapa Bongo, anamchukia Sintah kwa kuongea kitu asichokijua na kumponda yeye na Snura.

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole.
Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

                                                Sintah

No comments:

Post a Comment