Pages

Saturday, December 21, 2013

DIAMOND PLATINUMZ NA VJ PENNY WADAIWA KUMWAGANA.

Diamond Platinumz na Peniel Mungilwa(VJ Penny) wanadaiwa kumwagana huku moja ya sababu zikidaiwa ni Wema Sepetu na wawili hao(Penny na Diamond) kila mmoja kujiona yupo juu. Chanzo kimoja cha habari kiliiambia Globalpublishers kwa kusema................

 "Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
"Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?"


VJ Penny alipotafutwa na mtandao huo alionekana kutokuwa tayari kuliongelea suala hilo na kusema ataliogelea hivi karibuni "Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini."

Nae Diamond alipopigiwa simu na kutumiwa sms kuhusu habari za kumwagana na Penny hakujibu chochote.

                                                   Diamond na VJ Penny

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment