Pages

Saturday, November 23, 2013

VAD FILM PRODUCTIONS WAINGIA MIKATABA YA FILAMU NA KAMPUNI ZA NORDISK FILMS NA BOLIG AALBORG, WAFUNGUA AKAUNTI MPYA YOU TUBE BAADA YA KUFANYIWA HUJUMA.

Wasanii wa VAD Film Production ambao ni waafrika wanaoishi nchini Denmark wakiwa wamejikita katika utengenezaji wa filamu kwa kutumia Lugha ya Kiswahili ambayo ni moja wa urithi wa bara la Afrika wamefanikiwa kuanzisha akaunti nyingine ya mtandao wa You tube kuhusu kazi zao za filamu baada ya kufanyiwa hujuma na watu wasiojulikana huku mashabiki wa filamu zao wakilalamikia kitendo hicho cha kifedhuli. Akaunt mpya waliofugua You tube ambayo itakuwa ikiweka filamu na trailer za kazi zao inaitwa v.a.d film production hivyo kwa ambao walikuwa wanapata shida kuona kazi zao wanaweza kuanza kuziona sasa kama kawaida.

Kwa upande mwingine pia wasanii hao ambao wameonyesha moyo wa kutangaza Uafrika huko Ulaya kwa kutumia lugha ya Kiswahili ambayo inazungumzwa pia nchi za Scandinavia wameingia mkataba na kampuni ya Nordisk Films ambayo ni kampuni kubwa ya usambazaji filamu katika nchi za Scandinavia hivyo wataanza kufanya kazi na kampuni hiyo. Vile vile wasanii hao pia ambao wameshafanya kazi na wasanii wa Swahiliwood(Tanzania) kama vile Lucy Komba wameingia mkataba kuhusu maeneo ya location ya filamu watakazokuwa wanatengeneza na Bolig Aalborg ambalo ni shirika la nyumba la Nordjylland na picha hapo chini zinaonyesha wakati wasanii hao walipokutana na shirika hilo kuangalia nyumba zao mpya ambazo tayari wameshajenga na nyingine bado zinajengwa kwa ajili ya kutumia kama location wakati wa kutengeneza filamu.

VAD likiwa na maana ya Voice Of Africa In Denmark ilianzishwa mwaka 2011 na inapokewa msanii yeyote mwenye nia ya dhati katika kuitangaza Afrika kupitia sanaa ya filamu na mwenye kipaji cha uigizaji bila ubaguzi wowote.

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment