Friday, November 15, 2013

MCHINA AJITOSA KATIKA FILAMU ZA KITANZANIA AKIWA NA DR.CHENI NA SABBY ANGEL KATIKA FILAMU YA NIMEKUBALI KUOLEWA.

Filamu za kitanzania zinazidi kukua na kupendwa na watu wa aina na mataifa tofauti kila siku na sasa msanii mwenye asili ya China anayeitwa Chaoxiang Deming ( 朝翔 德明  ) ameamua kujitosa Swahiliwood akiwa na mastaa kama vile Muhsin Awadhi(Dr.Cheni) na Sabby Angel katika filamu mpya ya Nimekubali Kuolewa ambayo imeandaliwa na Dr.Cheni. Mchina huyo amecheza scenes akiwa anafumaniwa na kwa mujibu wake mwenyewe amesema ameamua kuonyesha kipaji chake pia katika filamu ili ajiongezee kipato kwani biashara kwasasa haziendi vizuri sana.

Ingawa mchina huyu sio raia wa kwanza wa kigeni wala kutoka china kucheza filamu za kitanzania lakini hii inahamasisha na kutoa changamoto kwa baadhi ya mastaa wa Tanzania ambao wamebweteka na walipofikia bila kujali ubunifu wala kuongeza elimu kuhusu tasnia ya filamu. Ikumbukwe kuwa Tanzania ni nchi yenye  wakazi na raia wenye asili ya mataifa mbalimbali hivyo suala la waigizaji wenye asili ya kiafika, kizungu, kihindi, kichina, kiarabu na mataifa mengine haliepukiki katika filamu zetu ambazo hutakiwa kuonyesha maisha ya kila siku. Mwangalie muigizaji huyo wa kichina katika filamu hiyo hapa Mchina Ajitosa katika filamu za Tanzania

Dr.Cheni na  Chaoxiang Deming ( 朝翔 德明  )

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment