Pages

Sunday, September 8, 2013

WASANII WA KIKE ACHENI KUVAA NUSU UCHI: JACKLINE WOLPER

Muigizaji wa filamu Swahiliwood Jackline Wolper amewaasa waigizaji wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo za nusu uchi kwani ni kinyume na mila na tamaduni za kitanzania na kiafrika kwa ujumla. Wolper aliyasema hayo kufuatia kupigiwa kura na kushinda kama muigizaji wa kike mwenye muonekano wa kistaa, akizungumza katika kipindi cha filamu cha Take One kinachorushwa Clouds Tv alisema yeye hawezi kuvaa mavazi ya nusu uchi ila anavaa yanayomsitiri mwili wake na bado anapendeza kuliko hao wanaovaa nusu uchi halafu hawapendezi."mimi nawakubali sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi, na ni kweli najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine"

                                   Wolper

 Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

1 comment: