Pages

Saturday, September 21, 2013

PASSPORT LOVE, FILAMU MPYA YA KISWAHILI NA KIINGEREZA KUTOKA DENMARK (PHOTOS).

Passport Love ni filamu mpya iliyotengenezwa nchini Denmark ikitumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Ni filamu fupi(short film) ambayo itatolewa You Tube baada ya wiki moja kuanzia sasa na baada ya mwezi mmoja uchukuaji wa filamu nzima utaanza rasmi. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni Devotha Alfred, Frank Salumu na Ace jack Lind na watengenezaji ni VAD Productions.

 Nilichokipenda katika watengenezaji wa filamu za kiswahili nje ya Tanzania/Afrika ni kuwashirikisha waigizaji wasio na asili ya kiafrika huku wazungu hao wakiongea kiswahili katika filamu hizo vizuri. Tunajisikia furaha zaidi kwa jinsi wasanii hawa wanavyozidi kuitangaza lugha ya kiswahili nje ya Afrika. Angalia baadhi ya exclusive picha za filamu hiyo fupi..........




Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment