|
Jackline Wolper |
Actress Jackline Wolper ambaye hakuna shaka kuwa kwa sasa ni kimbilio la maproducer wengi wa filamu Swahiliwood amefunguka kuhusu baadhi ya watu kumhusisha na tabia za usagaji (lesbianism) kwakuwa tu anapenda kuvaa mavazi yenye muonekano wa kiume wakati mwingine. Wolper amesema kuwa hata yeye habari hizo za chini chini zimekuwa zikimuumiza kwakuwa hazina ukweli wowote bali wabaya wake ndiyo wanaonekana kuzusha habari hizo. Muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto na mpenda fashions za aina mbali mbali alisema kuwa uvumi huo unamkera sana na itafikia hatua atawashitaki wote wanaomzushia kuwa ni msagaji(lesbian). Aliendelea lwa kusema kuwa mashabiki wake wamsikilize yeye na sio watu wengine kwakuwa yeye anapenda kuwa tofauti na hata fashions zake za nywele ni tofauti na mastaa wenzake wengine.
"Unajua kinachoonekana hapa ni watu
kutengeneza majungu juu yangu nataka ujue mimi kuvaa pensi na kuvaa nguo
kama zile(za kiume) haina maana ya kwamba mimi ni msagaji no mimi nina maisha
yangu na nina mtu wangu sasa haya sijui yanakujaje tena" alisema star huyo wa filamu za Ndoa Yangu, Dereva Tax na Tikisa na kuongeza kuwa "Mimi
kiukweli napenda sana kuwa tofauti na ndio maana ukiangalia styles za
nywele zangu wakati mwingi na nguo utagundua nipo tofauti sana sasa
naomba muchukulie nguo hizi ni nguo kama nguo nyingine msikariri jamani
mimi sio tom boy mimi ni Jack mwenye hisia na na homoni za kike na wala
sio msagaji. alimaliziaWolper akizungumza na thesuperstarstz
Wolper
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
dada jackline nakupenda sana napenda uwe dada yangu namba yangu kama hutojali 0684026980
ReplyDelete