Monday, September 2, 2013

AUNT EZEKIEL APONDWA NA MASTAA WENZAKE BAADA YA KUCHANWA KWA CHUPA.

Muigizaji wa filamu nchini Aunt Ezekiel amepondwa na baadhi ya mastaa wenzake baada ya kujeruhiwa mkono wake hivi karibuni na msichana mmoja anayeitwa Yvonne kisa kikidaiwa ni kugombea mwanaume mmoja aitwaye Jeff.  Mastaa wawili wa filamu jana kwa nyakati tofauti waliiambia Swahiliworldplanet kuwa wao pia hawajafurahia muigizaji mwenzao huyo kujeruhiwa ukifikiria kachimbwa vibaya na chupa mkononi ila wamesema Aunt kama mke wa mtu bado hajatulia kiasi cha kukumbwa na skendo za wanaume mara kwa mara licha ya kuwa kwenye ndoa. " me simtetei sana Anti licha ya kuumizwa, ye ni mke wa mtu tena mumewe anamuelewa kwa kazi zake za filamu hampi sana shida kama wanaume wengine wakishakuoa wanakuweka ndani na kuua kipaji chako, Anti kapata mume mwelewa ye anafanya mambo ya kujichafua kwa kuendekeza wanaume, tuliza kiranga bidada" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake kwa madai hataki malumbano na mtu.

Nae muigizaji mwingine wa kike ambaye tayari wameshacheza filamu kadhaa pamoja na Aunt kwa masharti ya kutotajwa jina alisema "Ajiangalie sasa ni mke wa mtu anajichafua mpaka ukweni na mwisho atampoteza mume huyo, Yvonne alikuwa anamlinda bwanake so siwezi mlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"

                                                     Aunt Ezekiel
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment