Stamina ambaye ni msanii wa hip hop nchini Tanzania na hit maker wa ngoma
kibao ambazo zinafanya poa sana, mojawapo ikiwa ngoma yake mpya(Mwambie Mwenzio)
aliyofanya na Darasa pamoja na mwanadada Warda anayesoma chuo kikuu
cha SAUT Mwanza amesema anakerwa sana na baadhi ya
wasanii ambao wamekuwa wakijihusisha na utumiaji au uuzaji wa dawa za
kulevya . Msanii huyo amesema inauma sana kuona baadhi ya wasanii
wanavyowachambua wenzao kwa kukamatwa na hayo madawa nje ya nchi kitu
ambacho kinafanya wasanii wengi waonekane kuwa ni watumiaji wa madawa hayo na kusababisha pia
usumbufu kwa wengine pale wanapotaka kusafiri kwenda nje kwa ajili ya
show . Stamina ameyasema hayo katika kipindi cha Strengo Saturday
kinachorushwa na radio Victoria fm iliyopo Musoma mkoani Mara, wakati akifanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale.
Hiyo ilitokea mara baada ya mazungumzo mengi tu ya utambulisho
wa kazi yake hiyo mpya aliyofanya na kina Darasa pamoja na Warda , na
mafanikio mengine ya kazi zake kimuziki. Mtangazaji huyo alimuuliza
kuhusiana na kashfa zilizopo katika mitandao ya kijamii pamoja na katika
vyombo vya habari ,kuhusiana na baadhi ya wasanii kukamatwa na madawa
ya kulevya wanapokuwa ughaibuni kupiga show . Stamina alisema "
unajua nini Patrick , mimi huwa naumizwa sana na hawa wasanii ambao
wanafanya hayo mambo maana wanatufanya hata sisi tusiohusika
kuonekana tunafanya hayo pale tunapokuwa nje ya nchi katika shows au
katika mambo binafsi. Aliendelea kusema kuwa wasanii wengi wanatamani
kuishi maisha ya juu kwa haraka haraka ndio maana unakuta wengi
wanapatwa na tamaa ya mambo amabyo hawana uwezo nayo, na mwisho wa
siku unakuta wanajiingiza katika biashara ambazo sizo , na mambo
yanayowaweka katika hatari kubwa.
Like our facebook page Swahili World Planet
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
No comments:
Post a Comment