Monday, August 26, 2013

OMEGA CONFUSION YAANZA KULETA MAPINDUZI KUTOKA KWA WASAMBAZAJI WANAOENDEKEZA UNYONYAJI.

Mtitu ambaye ni muigizaji maarufu na wa siku nyingi, pia director na producer ambaye ameibua vipaji vingi Swahiliwood ameandika hivi katika mtandao mmoja wa kijamii leo "
"OMEGA, historia mpya…
Leo tumeanza kuisambaza filamu yetu ya OMEGA na imepokelewa vizuri kiasi cha kutulazimu kuzalisha upya nakala nyingine masaa matano tu baada ya kuiingiza sokoni.
Nilipotangaza kujikwamua kutoka katika makucha ya wanyonyaji kwa kuanza kusambaza mwenyewe sinema zangu nilipokea kashfa nyingi sana kutoka kwa wasanii wenzangu hasa mastaa kuwa nitashindwa lakini sikurudi nyuma, nilikaza moyo na kuendelea na mkakati wangu.
Naomba watanzania wenzangu muendelee kuniunga mkono ili hata wenzangu wapate ujasiri wa kujikomboa.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru watendaji wote wa 5 Effects, waandishi wa habari, baadhi ya viongozi wa serikali, marafiki wa ndani na nje ya nchi kwa kuwa nami bega kwa bega katika uamuzi huu mgumu.
AHSANTENI SANA WATANZANIA WENZANGU KWA SAPOTI YENU.
By
William Mtitu"
Like our facebook pages Swahili World Planet Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment