Siku chache baada ya kutangaza kuanza kusambaza filamu, mkurugenzi wa kampuni ya 5Effects ametishiwa usalama na watu wasiojulikana.
Chanzo makini kimepenyeza habari Globalpublishers kuwa, Mtitu alipoingiza sokoni filamu yake ya Omega Confusion mapema Jumatatu hii ambapo ilidaiwa kuuza nakala zote siku hiyo hiyo kiasi cha kuzalisha nakala nyingine , watu wanaodaiwa kuwa ni wamiliki wa kampuni ya kusambaza kazi za wasanii wamemtishia kuwa wana mpango wa kumdhuru yeye ili asiendelee na kazi hiyo.
“Wamepitisha meseji ya vitisho kupitia kwa watu wao wa karibu ambao ni marafiki zangu, wakanitonya kuwa wana mpango wa kuniangamiza ili nisiwaharibie biashara yao,” alisema Mtitu na kuongeza:
“Kimsingi mimi simuogopi mtu, baada ya hii Omega natarajia kuingiza filamu ya Nyati ambayo itatoka siku si nyingi" alisema mtitu

Mtitu hivi karibuni aliweka wazi kuwa ameamua kusambaza filamu zake mwenyewe ili kuepuka unyonyaji wa wazi kutoka kwa wasambazaji ambapo wasanii wengi wamekuwa wakilalamikia hali hiyo kuwa mikataba ya filamu haiwafaidishi. Filamu yake ya Omega Confusion aliyoisambaza mwenyewe kuanzia jumatatu wiki hii inadaiwa kufanya vizuri sana sokoni kiasi cha nakala mpya kuzalishwa tena ili kuwafikia wanunuzi.
William Mtitu
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
No comments:
Post a Comment