Friday, August 23, 2013

LULU ATINGA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU KWA AJILI YA FOOLISH AGE (PHOTOS).

                                        LuluPIX 3Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”.PIX 1Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi. PIX 2Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.


……………………………………………………………

 Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

KAMPUNI ya Proin Promotions imewasilisha filamu yake iliyopewa jina la “Foolish Age” kwa Bodi ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukaguzi ambapo baada ya kufanyiwa marekebisho filamu hiyo inaweza kuruhusiwa katika uzinduzi wa Kampuni hiyo hivi karibuni.

Bodi ilifikia hatua ya kuwaita wahusika yaani Proin Promotions na Elizabeth Michael (Lulu) kwa ajili ya kufanya majadiliano kuhusu maudhui na maadili katika filamu hiyo kabla ya kufanyia maamuzi.

Katika majadiliano hayo Bodi ya Filamu iliwakumbusha wahusika hao kufanya baadhi ya marekebisho katika filamu hiyo ili iweze kuwa kivutio kwa umma, pia Bodi ya Filamu iliwakumbusha juu ya umuhimu wa kuzingatia kifungu cha 14 cha Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambacho kinaipa Bodi mamlaka ya kukagua filamu, matangazo na maelezo yote na kile cha 24 (1) (d, n na t) cha Kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kinachofafanua mambo yanayotakiwa na yale yasiyotakiwa katika filamu ambayo filamu hiyo imekwenda kinyume. Soma zaidi habari hii HAPA

 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

 

No comments:

Post a Comment