Filamu ya Foolish Age ya muigizaji Elizabeth Michael(Lulu) inadaiwa kukwama bodi ya filamu na michezo ya kuigiza kwa madai kuwa baadhi ya mavazi yaliyotumika humo ni kinyume na maadili ya mtanzania hivyo inahitaji marekebisho. Kwasasa inadaiwa wahusika wanafanya juu chini ili marekebisho hayo yafanyike haraka ili filamu hiyo izinduliwe tarehe 30 mwezi huu katika ukumbi wa Mlimany City kama ilivyopangwa. Filamu hiyo imewakutanisha mastaa kama Lulu, Diana Kimaro, Hashim Kambi na Jengua.
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
No comments:
Post a Comment