Wednesday, August 28, 2013

ALIYEMCHANA KWA CHUPA AUNT EZEKIEL NI HUYU HAPA.

Mwanamke mmoja amabye amejulikana kwa jina moja tu la Yvonne ndiye anayedaiwa kumchana kwa chupa muigizaji Aunt Ezekiel juzi usiku katika Club Billicanas. Inadaiwa siku za nyuma Aunt Ezekiel aliwahi kumchukulia Yvonne mwanaume wake na waliingia katika mzozo hivyo inawezekana Yvonne amelipiza kisasi ingawa Aunt alisema walishayamaliza. Yvonne alitaka kumpiga chupa ya uso Aunt sema akaiwahi kuizuia kwa mkono na ndiyo ikamchana. akizungumza na paparazi wa GPL alisema...........

"Risasi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?

Aunt: Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo maana ikaniumiza.

Risasi: Siku za nyuma uliwahi kuingia kwenye mzozo na Yvonne kwamba unamchukulia mpenzi wake aitwaye Joff, siyo kwamba ndiyo kisasi?

Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu."

Baada ya tukio hilo muigizaji huyo alienda hospitali kutibiwa na Yvonne anashikiliwa kituo cha polisi Oysterbay baada ya vurugu kubwa kuzuka ukumbini na show kusimama kwa muda.

                                              Yvonne

 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment