Monday, July 22, 2013

SINA MIMBA JAMANI NA KILICHOANDIKWA SIJAKIONGEA: ROSE NDAUKA

Baadhi ya mitandao tangu juzi imeandika kuwa muigizaji maarufu Swahiliwood Rose Ndauka huenda ana mimba baada ya  hivi karibuni kudaiwa kuugua ghafla alipokuwa location, na presha kumpanda pamoja na kichefuchefu wakati akishuti filamu yake mpya ya Jawabu na kupelekea kuomba msaada baada ya kujisikia vibaya. Baada ya habari hizo kuenea baadhi ya mashabiki wa muigizaji huyo mwenye kipaji cha kuigiza walituma ujumbe SWP ili kumuuliza star huyo kama ni kweli anatarajia kupata mtoto au lah. Hata hivyo Rose alipoulizwa na SWP alisema habari hizo sio za kweli na hana mimba. "sio kweli na kilichoandikwa sijakiongea"  alijibu kwa ufupi actress huyo aliyejaaliwa mvuto.

 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment