Thursday, July 4, 2013

MUIGIZAJI SULEIMAN BARAFU ASAINISHWA NA KAMPUNI YA LEO MEDIA.

Muigizaji maarufu nchini Suleiman Barafu amesainishwa mkataba na kampuni ya Leo Media ambapo mkataba huo wa miezi 12 ni kwa ajili ya muigizaji huyo kufanya kazi zake za filamu na kampuni hiyo na kusambazwa na kampuni hiyo hiyo. Hata hivyo bado mkataba huo unamruhusu muigizaji huyo kucheza filamu za wasanii au kampuni nyingine. Chini ni production manager wa Leo Media Geofrey Kusila ambaye pia ni muigizaji wa filamu akimsainisha Suleiman Barafu tayari kuanza kazi na Leo Media.


No comments:

Post a Comment