Pages

Wednesday, July 31, 2013

KUWEKA PART 1 NA PART 2 NI TATIZO SUGU KATIKA FILAMU ZA KIBONGO: DUDE

Muigizaji maarufu nchini Kulwa Kikumba(Dude) amekiri kuwa kuweka sehemu ya kwanza na ya pili(part 1na part 2) ni tatizo sugu katika filamu za kibongo. "Ni tatizo kweli" alisema Dude alipoulizwa kutoa maoni yake ingawa mwenyewe alipoulizwa na Swahiliworldplanet anadhani suluhisho la tatizo hilo ni nini alishindwa kujibu.

 Watengenezaji wengi wa filamu nchini wamekuwa wakitengeneza filamu kwa kuweka part 1 na part 2 huku story na scripts  nyingi zikiwa hazikidhi vigezo au muda wa kuigawanya filamu katika sehemu mbili kitu ambacho ni moja ya sababu kubwa kwa filamu za nchini kushindwa kutamba katika tuzo za kimataifa ikiwemo ZIFF kwani nyingi zinaonekana kuwa maigizo zaidi kuliko kuwa filamu. Utakuta filamu ina dakika 80 au 90 halafu inagawanywa katika sehemu mbili yaani part 1 na part 2 hii sio sahihi na pia ni wizi kwa walaji. Baadhi ya waandaaji wa filamu nchini wanadhani kununua vifaa vya kisasa pekee ndiyo kufanya filamu bora kumbe sivyo, kwani kutengeneza filamu bila kuigawanya katika sehemu mbili inahitaji vifaa vya kisasa pia ! Kitendo hiki pia ni ulipuaji wa kazi za filamu. Tubadilikeni wadau

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment