Pages

Friday, June 21, 2013

WEMA SEPETU NA KAJALA WATIBUANA !

Waigizaji wawili maarufu wa filamu Swahiliwood Wema Sepetu na Kajala Masanja wanadaiwa kutibuana. www.globalpublishers.info imeripoti baada chanzo kilicho karibu na wawili hao kutoa habari hizo kwa kusema kuwa baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya milioni 13 walikuwa marafiki wakubwa sana lakini kwasasa sio kama walivyokuwa mwanzoni. Inadaiwa kuwa kabla Kajala hajaenda Mwanza kwa mapumziko mafupi hivi karibuni siku moja aliamka lakini Madam(Wema) alikuwa kamchunia bila kujua sababu. Inadaiwa pia Kajala alipata deal la kwenda kucheza filamu nchini China na wasanii wenzake na kukamilisha taratibu zote huku baba yake akimruhusu lakini Wema alikataa Kajala kwenda China "Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu''

Inadaiwa kuwa chanzo ni mil. 13 alizolipiwa na Wema hivyo hatakiwi kucheza filamu za watu wengine licha ya Kajala kutegemea filamu ili aishi mjini " “Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?" kilisema chanzo hicho

Wema alipotafutwa kwenye simu yake hakupatikana lakini alipofuatwa meneja wake Martin Kadinda na kuulizwa kuhusu sakata hilo alijibu "Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu.
“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”. Meneja huyo alipoulizwa Wema anaumwa nini alisema hajui kwakuwa ugonjwa ni siri ya mgonjwa mwenyewe na daktari.

Mwandishi huyo wa GLB alifanikiwa kumpata Kajala kupitia simu yake ya mkononi na alipoulizwa kuhusu kutibuana na Wema huku sauti yake ikiwa ya chini alijibu "Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”. Hata hivyo inadaiwa kuna baadhi ya marafiki wa upande wa Kajala na wa upande wa Wema wamekuwa wakitia maneno maneno katika urafiki wa wawili hao licha ya kudaiwa kuwa sababu ni mil.13 alizolipiwa Kajala  ili asifungwe jela

                                Wema na Kajala

No comments:

Post a Comment