Pages

Saturday, June 22, 2013

NIKITA: SIPEWI NAFASI KATIKA FILAMU LABDA KWAKUWA SIVAI VIMINI NA SINA SKENDO ZA KUJIFANYIA PROMOTION.

Nimelazimika kuandika hapa kutokana na maoni niliyoyapata kutoka kwa muigizaji aliyetamba kipindi cha nyuma kidogo na mwenye kipaji cha uigizaji na mvuto pia. Huyu si mwingine bali Elizabeth Chijuba(Nikita). Nikita ametamba na filamu kadhaa nyingine akiwa na marehemu Steven Kanumba baadhi ya filamu hizo ni The Stolen Will, The Lost Twins, Copy na C.I.D na pia ana uwezo wa kucheza sehemu yoyote ile katika filamu na uhusika kumkaa vizuri. Hata hivyo muigizaji huyo kwasasa haonekani sana katika filamu mpya hivyo Swahiliworldplanet ililazimika kumuuliza hilo na jibu lake alisema haitwi na kupewa nafasi na watayarishaji wa filamu  labda kwakuwa havai vimini na kupata promo kwasababu ya kutokuwa na skendo akimaanisha kuwa anajiheshimu hivyo hawezi kujitafutia umaarufu wa skendo ili apate offer za kucheza filamu. "Sicastiwi sijui tatzo labda kwa vile sivai vimin na sipati promo labda kwakua cna skandol" alisema actress huyu mwenye dimples.

Alichokisema Nikita kina ukweli mkubwa ndani yake kwakuwa baadhi ya waigizaji wengi wanaotamba kwasasa wana skendo kila kukicha huku baadhi yao wakishindwa kuonyesha acting skills licha ya kucheza filamu kibao kila kukicha. Vile vile wapo baadhi ya waigizaji wachache sana ambao wanapata kazi za filamu licha ya kutokuwa na skendo. Baadhi ya waigizaji wanajitafutia skendo za makusudi ili waandikwe magazeti na kuwa maarufu ili wapate nafasi za kucheza filamu licha ya kutokuwa na vipaji. Ukiangalia alichosema Nikita kuna sababu kadhaa ambazo zinasababisha hali hiyo

1. Mfumo mbovu wa usambazaji. Ni kweli kuwa hakuna msambazaji  au muandaaji anayetaka kupata hasara lakini ni wazi mfumo ni mbaya. Baadhi ya waandaji na wasambazaji huwatumia wenye skendo ili kuuza hata kama hawana vipaji kitu ambacho kinaua industry badala ya kuikuza. Mfano kuna baadhi ya watengenezaji wa filamu nje ya Tanzania walionekano/wanaonekana kuvutiwa na baadhi ya mastaa wa filamu za Tanzania ili wafanye nao kazi kwakuwa ni maarufu na wanaadikwa kila mara kwenye media lakini wanapokutana nao na kuwajaribu vipaji havionekani hivyo kuwatosa na wao kuishia kusema bado deal la kucheza filamu nje ya nchi lipo kumbe kipaji chake hakijaonekana licha ya kuwa maarufu sababu ya skendo.

2. Magazeti ya udaku. Licha ya magazeti hayo kuwa na mchango mkubwa katika kuandika habari za kuelimisha na kufichua uchafu lakini ni wazi kuwa jinsi ya uandikaji wake wa skendo za wasanii huchangia tatizo la kutumia wasio na vipaji katika filamu badala ya wale wenye vipaji. Wakati media nyingi za nje zinampa kipaumbele star wa filamu kwa kazi zake lakini hapa kwetu magazeti ya udaku hushupalia skendo ili yauze. Magazeti haya yanafuata sana mfumo wa mastaa wa Hollywood jinsi wanavyoandikwa na media badala ya kuangalia kuwa sisi ni waafrika hivyo lazima tusitoe nafasi kubwa kwa baadhi ya habari ili kuua mfumo wake zisitokee tena lakini wapi. Tatizo la kushupalia skendo limefanya baadhi ya mastaa wa filamu Tz kuwa maarufu kupitiliza licha ya kutokuwa na vipaji hivyo kutumiwa katika filamu ili filamu ziuze, na wakati mwingine hutengeneza skendo kusudi ili waandikwe. Wale ambao wanajiheshimu na kutotaka skendo hawapewi nafasi kubwa katika media licha ya kuwa na kazi nzuri kuliko wenye skendo. Ni wazi kuwa media yakiwemo magazeti ni rahisi kuathiri kitu au mfumo kama tunavyoona sasa kwenye filamu. Waandishi wanashindwa kujifunza, kuna mastaa wanawaandika kila siku kwa nia ya kuwarekebisha kumbe wanazidi kuwapa kiburi cha kufanya skendo zaidi kwakuwa hawaogopi kuchafuka lengo lao ni kuwa maarufu tu. Wengine tayari wapo kwenye ndoa lakini hakuna nafuu kwasababu wanataka umaarufu na sio ndoa.

Tatizo hili la kuwatumia wauza sura wasio na vipaji kwa kulazimisha skendo litaisha kama magazeti yatabadilisha upepo wa namna ya kuwaandika mastaa. Yaani kama kuna skendo ya msanii basi isipewe nafasi   bali kazi za msanii ndiyo zijadiliwe na kupewa nafasi kwenye media. Kama filamu mpya ya muigizaji,director au producer imetoka magazeti yaandike performance au kazi yake kama ni nzuri au mbaya. kama ni nzuri  anaandikwa na atakuwa maarufu kwa kazi zake hivyo waandaji kumtaka katika kazi zao na hata wasambazaji watafurahia kazi zake. Na kama performance ya msanii ni mbaya basi hakuna kumbakisha, ni kueleza wazi na kwa wale wauza sura hawatapata nafasi tena kwakuwa skendo zitakuwa hazipewi nafasi tena hivyo watachuja na kuondoka kwenye industry.

Hii itasababisha kuleta maadili ya kazi kwa wasanii na jamii kwa ujumla na pia wasanii watapata heshima tofauti na sasa. Mfano media nyingi za Bollywood zinamuandika msanii kutokana na kazi zake na skendo hazipewi nafasi kutokana na jamii zao kuzingatia maadili, matokeo yake mastaa wengi wa Bollywood ni maarufu sababu ya kazi zao na sio skendo ni nadra sana kuona skendo sa wasanii wa Bollywood zikiandikwa na kama ni mfuatiliaji wa sinema zao basi hili unalijua. Pia kukosekana kwa professional film critics ni sababu mojawapo, hawa wangekuwa wanachambua na kuandika kazi za msanii na sio skendo au umaarufu wa mtu. Pia tuzo zikiwepo tatizo hili litapungua kwa maana wenye vipaji watatambulika na sio kama sasa.



         Akiwa na marehemu Steven Kanumba ambaye walicheza pamoja filamu kadhaa

No comments:

Post a Comment