Waigizaji wawili maarufu wa filamu Swahiliwood Wema Sepetu na Kajala Masanja wanadaiwa kutibuana. www.globalpublishers.info imeripoti baada chanzo kilicho karibu na wawili hao kutoa habari hizo kwa kusema kuwa baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya milioni 13 walikuwa marafiki wakubwa sana lakini kwasasa sio kama walivyokuwa mwanzoni. Inadaiwa kuwa kabla Kajala hajaenda Mwanza kwa mapumziko mafupi hivi karibuni siku moja aliamka lakini Madam(Wema) alikuwa kamchunia bila kujua sababu. Inadaiwa pia Kajala alipata deal la kwenda kucheza filamu nchini China na wasanii wenzake na kukamilisha taratibu zote huku baba yake akimruhusu lakini Wema alikataa Kajala kwenda China "Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi
tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa
kuwa alikataa kumruhusu''
Inadaiwa kuwa chanzo ni mil. 13 alizolipiwa na Wema hivyo hatakiwi kucheza filamu za watu wengine licha ya Kajala kutegemea filamu ili aishi mjini " “Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa
inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije
jamani?" kilisema chanzo hicho
Wema alipotafutwa kwenye simu yake hakupatikana lakini alipofuatwa meneja wake Martin Kadinda na kuulizwa kuhusu sakata hilo alijibu "Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika
tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu
yapo nje ya uwezo wangu.
“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa
lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini
sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na
kupelekwa hospitali.”. Meneja huyo alipoulizwa Wema anaumwa nini alisema hajui kwakuwa ugonjwa ni siri ya mgonjwa mwenyewe na daktari.
Mwandishi huyo wa GLB alifanikiwa kumpata Kajala kupitia simu yake ya mkononi na alipoulizwa kuhusu kutibuana na Wema huku sauti yake ikiwa ya chini alijibu "Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”. Hata hivyo inadaiwa kuna baadhi ya marafiki wa upande wa Kajala na wa upande wa Wema wamekuwa wakitia maneno maneno katika urafiki wa wawili hao licha ya kudaiwa kuwa sababu ni mil.13 alizolipiwa Kajala ili asifungwe jela
Wema na Kajala
No comments:
Post a Comment