Pages

Tuesday, June 25, 2013

SASA NI ZAMU YA RIYAMA ALLY KUONYESHA MCHARUKO WAKE.

Tegemea kumuona Riyama Ally akicheza kama msichana mcharuko katika filamu yake mpya inayokuja. Maudhui ya filamu hiyo ni ya dini(uislamu) lakini katika filamu hiyo Riyama anakuwa ametekwa na mambo ya kidunia zaidi na kusahau dini na kuudharau mwezi mtukufu wa Ramadhani. Swahiliworldplanet ilipomuuliza Riyama kuhusu character yake in the movie akiwa amecheza kama Zuwena alisema "ni msichana ambaye nimeikumbatia zaidi dunia kuliko dini na nimeisahau akhera ambayo ni maskani. nimecheza kwa jina la Zuwena, ni ya kiislam. siheshimu mafundisho ya dini yangu naudharau mwezi mtukufu wa ramadhani".

Hope filamu hii itakuwa na ujumbe mzuri maana wakati Riyama akiwa amecheza kama mcharuko Batuli yeye ameigiza kama mtu ambaye anafuata mafundisho ya dini yake. Mastaa wengine wa filamu hiyo ambayo jina lake bado kujulikana ni pamoja na Haji Adam(Baba Haji), Suleiman Barafu, Swebe, Patrick aliyetamba na filamu za marehemu Kanumba, Thecla Mjata, na Hidaya Njaidi. Hii picha ni kutoka filamu hiyo hapa anaonekana Riyama na Batuli........


1 comment: