Saturday, June 22, 2013

BATULI NA BABA HAJI WAJA NA FILAMU KWA AJILI YA MWEZI WA RAMADHANI.

Yobnesh Yusuph(Batuli) anakuja na filamu mpya kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mmoja wa mastaa wengine katika filamu hiyo ni Haji Adam(Baba Haji). Tumeshindwa kujua mapema jina la filamu hiyo lakini utapata upadates zake hapa hapa SWP. Mwaka jana pia Batuli alicheza katika filamu iliyozungumzia maudhui ya dini ya kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kucheza vizuri katika nafasi yake. Filamu hiyo ilikuwa Glory Of Ramadhani ambayo wengine waliocheza humo alikuwa Vicent Kigosi(Ray), Chuchu Hans, Halima Yahaya(Davina) na Dullah ambaye ni mtangazaji wa Channel 5 katika kipindi cha Planet Bongo.


No comments:

Post a Comment