Pages

Wednesday, May 22, 2013

WEMA SEPETU APONDWA KWA KUSEMA KIM KARDASHIAN NI IDOL WAKE NA ANAMPENDA SANA.

Wema Sepetu amesema kuwa anampenda Kim Kardashian na pia ni Idol wake hata hivyo kauli hiyo imewaacha midomo wazi baadhi ya watu kwakuwa Kim alikuwa Star wa picha za utupu mwanzoni na hata mitandao mingi ya marekani huwa inaandika haijui Kim ni star kutoka fani ipi hasa licha ya kuwa na Kipindi cha Keeping up with the Kardashians kwa kuwa mastaa wengi wa Hollywood wamo kwenye fani zinazotambulika sana, Amber Rose pia anawekwa kwenye kundi moja na Kim kuwa haijulikani umaarufu wake ni wa nini kwakuwa yeye pia yupo yupo tu licha ya kudaiwa ni model. Shabiki mmoja ameandika hivi katika page ya bongo5 "hw cn she be hr idol wen kim shz aporn star???...birds 04 same fthr flow 2gthr....shame on u wema hope u wnt be aporn actor". 

Ukiachana na shabiki huyo mtu mwingine aliyejitambulisha kama mdau wa filamu alisema kuwa Wema anaona Kim ni shost na Idol wake kwakuwa tabia zao zinakaribiana "she is rite n fame ya wema pia haitkani na films kwa kiasi kikbwa bt scandalz always" alisema mdau huyo kwa jina la Ibra. Ukiachana na maoni ya watu hao msichana mmoja kwa jina la Grace alisema kila mtu ana haki ya kupenda bila kujali anampenda nani "huwez mchagulia mtu kupenda au inspiration pengine wema is inspired by tabia za Kim"

                                                     Wema Sepetu

No comments:

Post a Comment