Pages

Tuesday, May 21, 2013

SELEMBE TOKO KUTIKISA NA LUCY KOMBA KATIKA MOVIE YA FROM TANZANIA TO DENMARK.

Ukizungumzia waigizaji wa filamu za kiswahili wanaotamba Denmark ni lazima ulitaje Jina la Selembe Toko ambaye anashirikiana kwa ukaribu na waafrika wenzake nchini humo katika kutangaza filamu za kiswahili barani Ulaya. Selembe anatokea Congo na tayari ameshacheza filamu nchini Denmark ya Moyo Wangu akiwa na Ashley Toto wa Kenya ambaye anaishi Germany na pia tayari ameigiza na Lucy Komba wa Swahiliwood katika filamu ya From Tanzania To Denmark ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mapema mwezi ujao nchini humo na kwasasa maandalizi ya uzinduzi huo yakiwa katika hatua za mwisho. Hiki ni kitu cha kuwapongeza sana waafrika wenzetu hawa kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kiafrika hasa Lugha ya kiswahili ambayo inazungumzwa na watu wengi sana katika bara la Afrika na pia usisahau kuwa wanashirikiana kwa karibu na wasanii wenzao nchini humo ambao hawana asili ya kiafrika. Look at his Photos................


1 comment: