Pages

Tuesday, May 21, 2013

JACKLINE WOLPER: KAMPUNI KUBWA HAZINA PESA ZA KUTULIPA NDIYO MAANA HAZITUTUMII KATIKA MATANGAZO YAO.

Tofauti na baadhi ya watu kudai kuwa skendo za mastaa ndiyo chanzo cha kutopata deals za matangazo kutoka makampuni makubwa nchini, lakini actress Jackline Wolper amepangua madai hayo kwa kusema kuwa makampuni hayo hayana pesa za kuwalipa ndiyo maana hayawatumii mastaa mara nyingi. Wolper aliyasema hayo SWP ilipomuuliza ni kwanini mastaa wengi wa Tz hawatumiwi na makampuni makubwa katika matangazo yao kama wenzao wa nje ambao hujiongezea mapato kupitia mikataba ya matangazo na makampuni makubwa ndipo sexy symbol huyo wa Swahiliwood aliposema hayo. Hata hivyo kauli zote mbili za wanaodai skendo ni chanzo zinaelekea kuwa kweli na hata kauli ya Wolper ina ukweli ndani yake kwakuwa wapo Mastaa kibao wa filamu, muziki na mitindo nchini wana majina makubwa na skendo hawana lakini bado hawatumiwi na kampuni kubwa katika matangazo.

 Makampuni huwa yanatumia watu wa kawaida huku ikidaiwa wanawalipa pesa ndogo sana na mastaa wachache sana wakiwemo hata wenye hizo skendo kutumiwa. Inadaiwa baadhi ya wasanii huwa wanafuatwa na kampuni hizo lakini huwa wanashindwa kuafikiana kwa kuwa pesa inakuwa ndogo sana huku sura zao zikitumika muda mrefu katika matangazo. Inadaiwa baadhi ya kampuni kubwa hutenga pesa nzuri lakini baadhi ya wafanyakazi wa vitengo husika hula pesa na kuchukua watu wasio na majina ili kuwatumia. Hata hivyo inadaiwa baadhi ya mastaa wachache licha ya kuwa na skendo lakini walishawahi kutumiwa na kampuni hizo kibiashara na kupata pesa nzuri mfano ukiwa mwanamuziki Diamond Platnumz.


No comments:

Post a Comment