Monday, May 6, 2013

RUGE AMJIBU JAYDEE, WATU WENGI BADO WAWA UPANDE WA JAYDEE, ANACONDA AAHIDI KUJIBU TENA MAPIGO.

Ruge Mutahaba ameamua kumjibu Lady Jaydee katika mkorogano wao na Clouds fm kuhusu suala la muziki wa Bongofleva, hata hivyo licha ya watu wengi kusoma na kusikia alichokisema Ruge kuhusu Jay Dee na muziki wa Bongofleva kwa ujumla asilimia kubwa ya watu mpaka sasa katika mitandao ya kijamii wanaonekana kuwa upande wa Jaydee na kuamni alichokisema huku madai na majibu ya Ruge yakishindwa kupewa uzito na wadau. Pia Jay dee ameahidi kuanika mambo mengine muda si mrefu. Katika ukurasa wake wa facebook ameandika hivi " Kama mtakumbuka niliahidi kutoa awamu ya pili tar 15 au 17 May na ahadi ni deni..Japo naona mbali ila Nitafanya hivyo, bado nina mengi sana ya kuzungumza kuhusu Ruge na wenzake...Ile ilikuwa ni trailer tu, Movie ndio linaanza sasa #TeamAnaconda no surrender". Katika ukurasa wa Bongo5 facebook wachangiaji wengi pia wameonekana kuwa upande wa Jaydee baada ya habari ya Ruge kumjibu Jaydee kuwekwa. Angalia twitter nako hawapo nyuma.............


No comments:

Post a Comment