Sunday, May 5, 2013

MOVIE REVIEW: MACHOZI YANGU

FILM: Machozi Yangu
DIRECTOR: Omary Clayton
CAST: Mohamed Musa, Slim Omar, Aunt Ezekiel, Hemed Suleiman
RATING: 1/5

Hii filamu ni moja ya mifano mizuri ya filamu mbovu na zisizo na kichwa wala miguu katika mambo mengi sana kitu kinachokuacha midomo wazi ilikuwaje mpaka watu wakakaa chini na kuitengeneza!. kwa ufupi ni kuwa haifai hata kuitwa mchezo wa kuigiza. Story yenyewe ya hii filamu haieleweki mwanzo, kati wala mwisho na imewekwa part 1 na part 2 huku muda ukiwa mdogo sana kama nusu saa tu kwa kila sehemu na hata kama ingekuwa na sehemu moja tu bila part 2 bado story ilikuwa haijitoshelezi kabisa huku ikionekana wazi ni ya kuunga unga. Screenplay nalo ni tatizo. Hata hivyo maajabu zaidi ni kwa director na editor, Omary Clayton kama muongozaji wa filamu hii ameishia kujitia aibu maana waigizaji ni kama vile walikuwa wakijiongoza wenyewe kwa kukosa director. Scenes na matendo ya waigizaji ni kituko tupu. Matukio ya uporaji yanayofanywa na Slim Omary na Clayton mwenyewe yalikosa mantiki na uhalisia mchana kweupeeee!. Mtu anaporwa na kupiga kelele huku kukiwa na vishindo tena karibu na madirisha na milango ya watu uswahilini lakini hakuna anayetoka halafu pembeni watu wanaonyeshwa wamekaa na kucheka na watu wengine wakichungulia na kuonyeshwa live huku vitendo vyenyewe vya hao waigizaji vikikosa uhalisia na nguvu kabisa. Mhariri wa hii filamu nae pengine ndiyo mara yake ya kwanza kushika computer kwakuwa hakuna alichokifanya cha maana huku scenes zikijirudia hovyo kutoka part 1 na part 2 bila mpangilio na akishindwa kuhariri matukio katika hii filamu kiasi kwamba mtu unaweza kudhani ilikuwa rehearsal ya kujiandaa kwenda kushuti filamu kumbe ndiyo filamu yenyewe!. Picha za filamu nazo hazikuwa na ubora wala kutulia vizuri kuonyesha pia cameraman hakua ametulia wakati akichukua picha za filamu hii.

Waigizaji nao licha ya kuwa na majina makubwa kama vile Aunt Ezekiel, Hemed Suleiman, Slim Omar na Mohamed Fungafunga(Jengua) waliishia kuwa vituko katika hii filamu kwa kutoa performance mbaya. Hata hivyo Bi.Fetty licha ya kuonyeshwa sehemu ndogo tu kama mke anayenyanyaswa na mume wake(Mohamed Fungafunga) alikuwa vizuri katika performance yake na pia Mohamed Musa kama muigizaji mkuu wa hii filamu kipaji chake hakijifichi hivyo akiendelea kuongeza bidii na kucheza katika filamu nzuri zijazo atakuwa na mafanikio baadaye. Aunt Ezekiel akiwa polisi katika tukio la kuonana na ndugu yake baada ya miaka mingi kupita hakuonyesha hisia zozote zile za kuuvaa uhalisia. Hemed katika hii filamu aliishia kutalii huku mavazi ya Aunt Ezekiel na muonekano wa Hemed akiwa na vipuli masikioni vikikosa mantiki yoyote. Kwa ujumla hii ni moja ya filamu mbaya sana za mwaka na zilizowahi kutengenezwa Swahiliwood.

No comments:

Post a Comment