Actor wa siku nyingi katika tasnia ya filamu na maigizo nchini Muhsin Awadhi(Dr.Cheni) amelishwa sumu yenye lengo la kumdhuru. Akizungumza na mtandao wa bongomovies the popular actor alisema kuwa sumu hiyo alilishwa wiki iliyopita katika harusi ambayo yeye alikuwa MC, alisema kuwa mmoja wa wahudumu hao alimpa chakula na baada ya kula akaanza kujisikia vibaya na kutoka nje na kuishia kutapika.Aliongeza kuwa alidhani ni vidonda vya tumbo hivyo aliamua kununua maziwa lakini alipopelekwa hospitalini aliambiwa kuwa amelishwa chakula chenye sumu. Dr. Cheni muigizaji mwenye moyo wa kipekee kusaidia waigizaji wenzake wanapokuwa katika matatizo alisema mpaka sasa hajui watu hao ni kina nani lakini akasema watakuwa wanamjua na lengo lao sio zuri kwake. Sasa hivi anaendelea vizuri na Lulu alikuwa mmoja ya watu waliofika mapema hospitalini kumjulia hali na kumpa pole.
Wiki kadhaa nyuma mwigizaji mwingine Husna Poshy(Dotnata) alilishwa sumu ya kumuua taratibu na watu wasiojulikana na hayo yaligundulika alipopelekwa hospitalini.
Pole sana Dr. Cheni mungu yuko upande wako na atawahukumu watu wa namna hii wasio na utu.
No comments:
Post a Comment