Pages

Tuesday, May 28, 2013

FILM REVIEW: NGUVU YA IMANI

FILM: Nguvu Ya Imani
DIRECTOR: Jackson Kabirigi
CAST: Julieth Samson(Kemmy), Simon Mwapagata(Rado), Jackson Kabirigi, Hadija Mohamed.
RATING: 2.5/5
 Filamu inazungumzia mfumo dume kwa kiasi kikumbwa. Kemmy ni mwanamke mjamzito huku akiwa mchapakazi, yeye na mume wake(Rado) wanafuga ng'ombe huku Kemmy akiwa muwajibikaji mkubwa kwa kuchunga ng'ombe, kukamua maziwa na kwenda kuyauza ili yeye, mumewe na mdogo wake(Jackson Kabirigi) ambaye ni mwanafunzi wapate kuishi. Hata hivyo licha ya kufanya yote hayo likiwemo jukumu la kumlipia ada mdogo wake, mumewe(Rado) anamnyang'anya pesa zote baada ya kutoka kuuza maziwa huku akimtuhumu kuwa ni malaya anapewa pesa na wanaume wengine. Vile vile Kemmy ni mgonjwa wa pumu ambayo humbana mara kwa mara huku bila kujali mumewe anampiga mateke ya tumboni mara kwa mara licha ya kuwa mjamzito, lakini nguvu kubwa ya Kemmy maishani ni kumtanguliza mungu katika kila akifanyacho. Kutokana na na kuwa na nguvu kubwa ya imani siku moja mwanga na sauti flani vinamjia vikimtaka awe mtumishi wa mungu ili kusaidia wengine wenye matatizo na hatimaye anakuwa mchungaji baada ya kufukuzwa na mumuwe aliyeamua kutembea na jirani yake(Hadija Mohamed) kwa nguvu za kishirikina.

Licha ya hadithi kugusa moja kwa moja maisha ya wanawake wengi wa kiafrika ikiwemo Tanzania kwa kufanya kazi sana huku waume zao wakiwanyanyasa lakini screenplay ya hii filamu haikuwa nzuri kwakuwa baadhi ya matukio yanakuacha na maswali kichwani baada ya kuangalia. Picha za filamu zilikuwa choice nzuri lakini tatizo lilikuwa katika mwanga, baadhi ya scenes picha zilikuwa na giza licha ya kuwa sio usiku. mfano scene iliyoonyesha wanafunzi wakiwa shuleni mstarini asubuhi. Direction ya hii filamu pia haikuwa nzuri kwa asilimia kubwa na ni rahisi kuona hasa kupitia performance mbaya ya Rado.

Kuhusu performances za waigizaji Kemmy alitoa performance nzuri kiasi cha kukushawishi kuendelea kuingalia filamu hasa kuanzia mwanzo mpaka kuelekea mwisho wa filamu. Hadija Mohamedi aliyecheza kama jirani wa kemmy na kutembea na mumewe pia alicheza vizuri bila kusahau yule mama mchawi. Jackson Kabirigi alikuwa kawaida huku akionekana kutumia nguvu nyingi katika uhusika wake bila maana ya msingi. Hata hivyo licha ya story kuwa na wazo zuri na performance ya Kemmy ikikushawishi kuangalia filamu hii, lakini ni Simon Mwapagata(Rado) ambaye performance yake mbaya ilifanya filamu ikose nguvu na mvuto kila anapoonyeshwa. Uhusika wa Rado ulitaka mtu serious na mkatili hasa lakini yeye alikuwa hayupo serious kwa kuweka vichekesho vingi hivyo hata director hapa alikosea kwa kutokuwa makini hata kama script ilitaka hivyo kwakuwa character ya kemmy na Rado zilishindwa kuchangamana kabisa. Rado anapokuwa serious au anapocheza kama adui hufanya vizuri lakini performances zake nyingi katika nafasi ya comedy huwa mbovu.

Kama hujaiona filamu hii itafute utafurahia zaidi character ya Kemmy kwa jinsi ilivyobeba ujumbe mzuri huku performance yake ikiwa ya kuvutia pia.

No comments:

Post a Comment