Friday, April 12, 2013

THEN & NOW: AUNT EZEKIEL

Katika harakati zake za kuusaka umaarufu Aunt Ezekiel alianzia katika mashindano ya urembo huko Mwanza na hatimae kupata tiketi ya kuingia Miss Tanzania mwaka 2006 ingawa hakufanya vizuri. Baada ya hapo alijitosa kwenye films akianzia na filamu ya Miss Bongo.

THEN: picha hii inamuonyesha Aunt akiwa katika harakati zake za awali katika showbiz, alikuwa bado na umbo lake la kimiss na wala hakuwa sista duu kivile wala mjanja wa mjini sana kama leo.

NOW: hivi ndivyo alivyo sasa actress huyu akiwa amenenepa na kuwa mdada wa mjini zaidi. picha zote mbili zinamuonyesha Aunt akiwa na ngozi ile ile na mavazi mafupi kama kawaida licha ya sasa kuwa mke wa mtu lakini kimavazi hajabadilika. Umaarufu wake ni mkubwa now kushinda enzi hizo, huku akiwa na skendo lukuki kuliko awali.

No comments:

Post a Comment