Wednesday, April 3, 2013

KAJALA AJICHORA TATTOO YA JINA LA WEMA, WATU WAMPONDA, WEMA NAE AJICHORA TATTOO MPYA YA KICHINA.

Actress Kajala Masanja ambaye hivi karibuni alitolewa mil.13 na Wema Sepetu kama faini yake ili asifungwe ameamua kujichora tattoo yenye jina la Wema kama ishara ya kumshukuru muigzaji huyo. Kajala amejichora tattoo hiyo mgongoni mwake upande wa kushoto. Hata hivyo baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake wamemponda kajala kwa uamuzi wake wa kujichora tattoo ya Wema kuwa hakufikiria mara mbili kama kweli alikuwa na nia ya kumshukuru kwa kuwa michoro hiyo kitaalam inadaiwa kuwa na madhara katika ngozi ya mhusika ikiwemo kusababisha kansa, pia wamesema hicho ni kitu cha muda tu so Kajala angefikiria mbali zaidi hata baadaye akijaaliwa kupata mtoto mwingine ampe jina la Wema au kitu kingine cha kudumu kuonyesha heshima na shukrani lakini si kujichora tattoo wakidai ni tamaduni za magharibi na ukichukulia issue aliyokuwa nayo mahakamani ilikuwa serious sana. Actress mmoja aliye karibu na Wema na Kajala kwa sharti la kutotajwa jina lake aliiambia Swahiliworldplanet "cjaona point alofanya Kajala kwa kujchora tattoo, ni kuiga uzungu tu instead angefanya cha maana zaid hata kumpa mwanae jina la Wema leta on", shabik mwingine kwa jina la Ismail alisema "am nt sure na alichofnya kajala cuz naona tattoo c isue". Licha ya hayo wengine wamechukulia poa tu kwa alichokifanya Kajala. Wema mwenyewe baada ya kuona kajala kajichora jina lake aliandika haya.
Kwa upande mwingne tena Wema Mwenyewe nae amejichora tattoo mpya yenye maneno ya Kichina mgongoni ingawa SWP ilishindwa kujua mara moja maana yake ni nini au pia ni jina lake kwa kichina. angalia tattoo ya Kajala na Wema hapo chini..................

                                                                              Kajala
                               Wema Sepetu na tattoo ya kichina

No comments:

Post a Comment