Monday, April 15, 2013

ISABELA MPANDA KUSHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE NDANI YA BOTI LEO HII NA MASTAA WENZAKE KIBAO.

Leo ni birthday ya Isabela mpanda ambaye ni actress na bongofleva singer, kama kawaida unavyojua Isabela ni mtu wa matukio basi habari zisizo na shaka kutoka kwake mwenyewe ni kuwa birthday yake itafanyika ndani ya Boti leo hii  huku mastaa wenzake kibao wakitarajiwa kuhudhuria kama vile Jini Kabula, Luteni Karama ambaye ni mpenzi wa Isabela, Jackline Pentezel(Jack wa Chuzi) Ngwear, dully, Baby Madaha, Mchizi mox, Daz Baba, H. Baba na mchumba wake Florah Mvungi . Isabela star mwenye makeke mengi pia amewataka mashabiki wake waendelee kumsapoti katika kazi zake za films na muziki kwa kuwataka wasikilize wimbo wake mpya wa "Nchi yetu" ambao ameuimba na members wenzake wa kundi la Scorpion girls, pia film yake mpya ya Tatakoa inatarajiwa kuingia sokoni wiki ijayo. Picha za birthday ya star huyo utazipata hapa hapa endelea kusoma blog hii.

                                                   HAPPY BIRTHDAY ISABELA

No comments:

Post a Comment