Pages

Sunday, April 28, 2013

"HATIA" FILAMU YA KITANZANIA ILIYOTAKIWA KUPELEKWA KWENYE TUZO NA MATAMASHA YA KIMATAIFA.

Nimeangalia filamu ya Swahiliwood inayoitwa HATIA ambayo ilitoka mwaka jana na nikiri kuwa ni moja ya filamu chache nzuri za Swahiliwood kwa mambo mengi. Kwanza story ya filamu ni nzuri na imejaa uhalisia wa maisha ya kiafrika na kitanzania, pia story yake siyo ya mapenzi bali shida za familia, unyanyasaji kutoka kwa vyombo vya dola kama vile polisi, na dhuluma kutoka kwa baadhi ya wanajamii. Filamu hii imetengenezwa na kampuni ya Timamu Effects na kuongozwa na Kulwa Kikumba(Dude) huku muigizaji mkuu akiwa ni Hisani Muya(Tino) na mama yake ambaye ni Bi. Aisha ambao performances zao ni nzuri sana hasa Tino jinsi anavyopigana na maisha magumu ya kijijini na baadaye mjini ambako anakumbana na dhuluma, unyanyasaji na uonevu mwingi bila kukata tamaa ya maisha huku mwishowe akibambikiwa kesi na ya mauaji bila haki kutendeka kitu ambacho kipo katika maisha ya watanzania na waafrika wengi kubambikiwa kesi na polisi ambazo hawahusiki nazo. Location zilikuwa nzuri kwa asilimia kubwa. Picha za hii filamu pia zilikuwa choice nzuri, huku mtu wa make up na mavazi akiwa amejitahidi sana katika filamu hii. Tino alicheza uhusika wa aina mbili kama mzee na kijana. Muongozaji Kulwa kikumba pia amefanya kazi nzuri kiasi kwamba ni vigumu kutambua makosa haraka katika hii filamu ingawa kuna location hasa za mahakama kama haikuwa choice nzuri lakini ukweli tunaujua kuwa bado kuna ugumu katika kupata location kutoka taasisi za serikali.

Niseme tu kuwa hii filamu ilistahili pia kupelekwa kwenye film festivals mbali mbali na ingeweza hata kushinda baadhi ya vipengele lakini tatizo watengenezaji wetu wa filamu wengi hawajui faida za film festivals hivyo hawaoni umuhimu wa kuzipeleka kazi zao. Hii filamu ingeweza hata kupata tuzo ZIFF, AMAA na hata matamasha ya filamu nje ya Africa ingeweza kupata baadhi ya tuzo. Niseme kuwa hata kama waandaaji wangejaribu kuipeleka katika Tuzo za Oscar ingekuwa jambo zuri hata kama isingepenya lakini ni vizuri kujua nafasi yetu kwa kile tunachotengeneza kwani filamu nyingine zinazopata tuzo za kimataifa zipo kwaida tu. Hata hivyo waandaaji hawajachelewa bado kuna film festivals na award functions wanaweza kuipeleka na kushinda. Tino na Bi. Aisha walistahili nominations ya tuzo, muongozaji, costume and make up designer pia walistahili nominations bila kusahau best picha. Hongera sana kwa watengenezaji na waigizaji wa HATIA.

                                                             Hisani Muya(Tino)

No comments:

Post a Comment