Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana
Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia
yoyote na ukurasa huu au watu hawa.
Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana
Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya
Uanamitindo popote pale.
Ukurasa halisi wa Flaviana Matata kwenye mtandaomwa wa Facebook ni Flaviana Lavvy Matata.
Hivi sasa tunaendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa
kuhusu uhalifu huu na tunaomba ushirikiano wenu pia Wanajamii.
Imetolewa na
Compass Communications
Maelezo zaidi wasiliana na Maria Sarungi mariast@compass-tz.com, +255 22 2182405
No comments:
Post a Comment